Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Ni Jumapili tulivu ambayo ni siku ya Wanawake duniani.Katika Taifa letu Wanawake wa Chadema wanafanya Kongamano lao kubwa katika Ukumbi wa Mlimani City DSM.

Idadi kubwa ya wawakilishi wa Wanawake wa Chadema kutoka mikoa yote tayari wako DSM kuhudhuria Kongamano hili.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hili anatarajiwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikael Mbowe.

Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.

---------------------------------------------------

Ukumbi wa Mlimani City linakofanyika Kongamano hili kumepambwa vema huku akina mama wakiwa wanawasili kwa wingi maeneo haya wakiwa na sare maalum za chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.

Ni furaha sana na shangwe kuu zimetanda hapa.Wengi wakijaribu kudadisi yatakayotokea hapa ikiwemo Hotuba inayosubiriwa kwa hamu ya mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Freeman Mbowe.ikumbukwe Mbowe aralihutubia Taifa kupitia Kongamano hili ikiwa ni siku moja kabla ya hukumu ya kesi ya kisiasa dhidi ya wanasiasa wakuu wa upinzani nchini.Wananchi wengi wakidhani hukumu hii huenda ikawa ndiyo kipimo cha imani ya wananchi dhidi ya mahakama hususan tuhuma za kuingiliwa na serikali.

Updates at 12.20pm

Sasa ndiyo viongozi wakuu wanaingia hapa Ukumbini.Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,Katibu Mkuu John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu Bara Benson Kigaila wakisindikizwa na Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee na viongozi wote wa Bawacha anapokelewa kwa shangwe kuu hoi hoi na nderemo.Wanawake wanampokea kiongozi wao kwa nyimbo za hamasa za kimapinduzi.

Kati ya watu mashuhuri waliohudhuria kongamano hili ni mwanaharakati maarufu Maria Sarungi Tsehai na Shangazi Fatma Karume mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume.Pia yumo Dr Azavel Lwaitama.

Limefuatia tukio la kuombea kongamano hili kutoka wawakilishi wa dini ya Kiislamu na Kikristo.Na baada ya hapo Katibu wa uenezi wa Bawacha Agnesta Lambert anatoa utambulisho kutoka mkoa kwa mkoa.

Baada ya hapo anakaribishwa Katibu Mkuu Bawacha Grace Tendega ambaye anatoa salaam za Baraza kisha anawaita wageni mbalimbali kutoka vyama vya siasa kuja kutoa salaam

Sasa anahutubia Mwenyekiti wa Bawacha Taifa Halima Mdee.Anapongeza wanawake wa Chadema kwa Jinsi walivyojipanga.Anaeleza mambo mbalimbali yaliyofanyika na kwamba leo itazinduliwa sera maalum ya Wanawake

Mdee anazungumzia changamoto nyingi zinazohusu wanawake zikiwemo Ajira,Afya,mikopo,elimu na Uongozi.Halima anasema serikali iliyoko madarakani imeshindwa kabisa kutatua changamoto za wanawake

Halima Mdee amelaani vikali sana Kauli ya Katibu Mkuu CCM Bashiru Ally kwamba CCM itashinda uchaguzi kwa kutumia dola.Mdee amesema kamwe wanawake hawatakubali na kwamba watanzania ndiyo wanaoweka serikali na si nguvu ya dola.Mdee amemhakikishia Mwenyekiti Freeman Mbowe kwamba Chadema itashinda kwa nguvu ya umma

Updates saa 2.35pm

Freeman Mbowe ndiyo anakaribishwa sasa kulihutubia Kongamano na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti Mbowe amezungumzua mambo makubwa matano.

Jambo la kwanza ni Ziara ya viongozi wa kisiasa Ikulu.Mbowe amesema yeye ama Chadema haijaalikwa na suala la msingi siyo Chadema kualikwa bali ni kwenda kufanya nini.Mbowe amesema hataki kwenda Ikulu kuzungumzia mambo yasiyo ya msingi bali anataka akiitwa Ikulu Rais ajue ajenfa kuu za Chadema ni Tume Huru ya Uchaguzi na Maridhiano ya kitaifa

Jambo la Pili, Mwenyekiti Mbowe amezungumzia Barua kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa kwenda kwa vyama vyote kuhakiki uhai wao ili kutambua vyama vinavyostahili kushiriki uchaguzi.Mwenyekiti ameshangazwa na Barua hiyo ya Msajili na kuhoji atawezaje kufanya uhakiki huku akijua kwa zaidi ya miaka minne na Nusu vyama vimezuiwa kufanya shughuli za kisiasa.

Jambo la Tatu, Mwenyekiti Mbowe amelaani vikali Tabia inayoshamiri ya watu wachache kutaka kutumia Ukabila kuligawa Taifa.Mbowe amesema kuna kikundi cha watu kimekuwa kikisambaza Taarifa zake kupitia mitandao ya kijamii kwamba kitatumia njia zozote kulinda kabila lao la Kisukumu na kumlinda Rais aliyepo.Mbowe ameonya vikali hali hiyo na kusema kikundi hicho kikiachwa bila kuchukuliwa hatua kitaligawa Taifa.

Jambo la nne, Mbowe amezungumzia ushirikiano wa vyama na kusema chana chake kinathamini sana ushirikiabo na kitakuwa tayari kushirikiana na chama chochote chenye nia thabiti ya kulikomboa Taifa.

Jambo la tano, Mbowe alikemea vikali kauli ya hatari na ya kibabe iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally kwamba chama chake kitatumia Dola kushinda uchaguzi.Mwenyekiti huyo amesema alikuwa anamheshimu sana Bashiru Ally kama mwanazuoni aliyebobea lakini anajidhalilisha kwa sababu tu ya ulevi wa madaraka.Mbowe amemtaka kwa hatua ya sasa Bashiru Ally atoke hadharani afute kauli yake na aliombe radhi Taifa.

Baada ya hotuba ya Mbowe iliyotizamwa na wachambuzi wa mambo kama Hotuba bora zaidi kwa mwaka huu amezindua rasmi sera za Chadema zinazohusu wanawake.Kisha aliondoka ukumbini na ujumbe wake kuruhusu wanawake kuendelea na kongamano lao kujadili mambo yanayowahusu.Kutakuwa na watia mada kadhaa wakiwemo Mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai, Rais wa zamani wa TLS Fatma Karume pia Mkurugenzi wa zamani wa LHRC Hellen Kijo Bisimba wanazuoni kadhaa kutoka Chuo kikuu cha DSM wakitoa mada kuhusu Ujasriamali,Haki za Binadamu,Katiba na sheria nk.

IMG-20200308-WA0048.jpg

IMG-20200308-WA0057.jpg

IMG-20200308-WA0058.jpg

IMG-20200308-WA0059.jpg


 
Ni Jumapili tulivu ambayo ni siku ya Wanawake duniani.Katika Taifa letu Wanawake wa Chadema wanafanya Kongamano lao kubwa katika Ukumbi wa Mlimani City DSM.

Idadi kubwa ya wawakilishi wa Wanawake wa Chadema kutoka mikoa yote tayari wako DSM kuhudhuria Kongamano hili.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hili anatarajiwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikael Mbowe.

Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.
Kwani polisi watakuwa likizo?
 
Mwenyekiti BAWACHA Mh Halima Mdee bila Shaka Ni Mnyama! 😉 😋
 
Ni Jumapili tulivu ambayo ni siku ya Wanawake duniani.Katika Taifa letu Wanawake wa Chadema wanafanya Kongamano lao kubwa katika Ukumbi wa Mlimani City DSM.

Idadi kubwa ya wawakilishi wa Wanawake wa Chadema kutoka mikoa yote tayari wako DSM kuhudhuria Kongamano hili.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hili anatarajiwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikael Mbowe.

Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.
Kibali cha kufanya mkutano mnacho bwashee?
 
Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.
Mkuu Molemo, kwanza asante kutuhabarisha and it's good to learn kuhusu Molemo Media, natumaini utatuletea live kupitia live streaming, naona kama umebeba mikoba ya Tumaini Makene, maana simsikii au na yeye ameisha jitambua?.

Hiki unachofanya sasa ndicho tulichowashauri mfanye toka ile 2015, mu invest into mass mobilization strategies za reaching out to reach the masses, mlipaswa muwe na redio yenu, TV yenu na interactive online media ya chama kabisa na sio kutegemea individual efforts.

Jamaa yangu alipokuja ile 2015 nilikuwa na matumaini makubwa
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Hata hivyo asante kutuhabarisha.
P
 
Back
Top Bottom