Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yapo kote mpk Dar sema Sio kiwango kikubwa ,walimu wengi tuna shida na tunapenda sana sifa tunadhani kuchapa ndo kufunza
Vijijini Huko Hali ni mbaya sana kwanza wakuu wa Shule wanajiona wao exceptional hawaguswi wanaanzisha masheria ya hovyo mashulenu watoto wanafukuzwa Shule kirahisi TU
Hapa Dodoma Shule Fulani siku ya mtihani wa darasa la 7 mkuu wa Shule kafukuza watoto wasifanye necta kisa hawajaja Shule wiki Moja TU,mpk wanafuni wenzao wakawa wanalalamika yaani wiki Moja mwl mkuu kafukuza wasifanye mtihani na anajua wazazi au walezi hawana uwezo wa kufatilia ipasavyo kutafuta hakiza watoto wao

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Daaah! Hii ni hatari na wazazi wenyewe hali za maisha duni. Hawawezi hata kufikisha malalamiko yao sehemu za juu maana hakuna anayewasikiliza. Daah inasikitisha
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?????

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.

View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
OMG!, huu ni zaidi ya ukatili.
 
Kuwa mwalimu Kama hiko kitu kinawezekana uone, mwalimu ana wajibu wa kitaaluma na nidhamu pia hio ni wajibi na lazima Hapo kwenye nidhamu Sasa nakwambia jaribu kuomba nafasi ya kuwa mwalimu hata kwa miezi mitatu then uwone sawa na useme wewe una wajibu wa nidhamu ya watoto wako eti huwezii wakiza tu watoto mpaka wanakua bila hata kuwafanya chochote impossible impossible
Mimi ni mwl 12+yrs plus ila Sina ujasiri wa kupiga mtoto hvyo,naadhibu inapostahiki ,nashirikisha wazazi 100%kwa Kila mtoto ,nawajua wanafunzi wanguu wore nnaowafundisha ukizingua nadeal na wewe kama inavyostahiki ila Sio kupiga kama naua nyoka,mkuu wa Shule akitaka taarifa za mwanafunzi yoyote msumbufu ananiita Mimi kwanza nimueleze then ndo hukumu zinatoka
Hawa watoto wanatoka backgrounds tofauti hatujwa walimu tuwafanyie ukatili,au tulipize tulivyofanyiwa tuko pale kama walezi,wazazi na washauri wao
Sipo kazini Kwa sasa watoto wananimiss juzi mmeenda mmekutana na watoto waeacha Shule Kwa visa TU vya walimu nimeumia mnooo, wanafunzi wananiambia madam ungekuepo ningemaliza Shule Mimi ila daahh mwl Fulani Ndo kasababisha nsimalize Mimi,walimu sisi wengi ni wakatili Mimi nachokipigania mwanafunzi yoyote yule hata awe mvuta bangi ukimtreat fair anakuelewa vzr Sema walimu hatuna saikolojia ya kweli
Wanafunzi wanapigana Mimi nikifika wanaacha,wanafunzi wa form 1 wanaporwa wakija kushtaki naenda Kwa wale wezi wa vidato vya juu huko machimboni nikifika wakiniona utaskia"oohh dogo katuchomesha shika begi Lako bwana hutaniwi"

Nakataa ukatili wa kijinsia Kwa wanafunzi walimua tuache

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hayo mamlaka mkuu wa shule anayatoa wapi? Tatizo ni kupewa vyeo kwa kuhonga ila kichwani hamna kitu.

Sent from my CPH2239 using JamiiForums mobile app
Anayatoa kwake mwenyewe Kwa maamuzi yake wakuu wa Shule wanajichukulia sana sheria mkononi,wananyanyasa sana wanafunzi na wazazi haswaa wakiona huna nguvu,kinachosaidia sehemu kama Dar uelewa ni mkubwa ila mikoani Hali ni mbaya sana
Yanatokea na yapo pia mengi maovu TU,mwl anaweza mrudisha Mtoto darasa kirahisi tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kama mwanao nilisugu wakwetu hawawezi kupigwa ivyo adhabu zipo na sheri mahali pakuchapa panajulikana kwaiyo ww unaona anapo chapa ni sahihi??????
Kwani amekufa?,mbona watu wanapigwa kwenye viganja na hamsemi,sasa kiganjani na unyayoni kuna utofaut gan
 
Mm siwez nikawa hapo staff nikavumilia icho kinacho tendeka....ova!
Japo sometimes hao watoto wanaweza kukupiga tukio mpka ukapanic.....
Mbona wazungu walisha abolished Stick in their school....
All in all Mungu ni mwema na Mwaminifu wakati wote.....
Usilete habari za wazungu hapa Tandale
Mkuu
Pamoja na kila kitu lakini kumfukuza mwalimu kazi ni kumkosea

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Askari nao vituoni humo huwa wapiga watuhumiwa hivihivi but sijawahi ona waziri was mkuu was mkoa akikemea?
 
Mimi ni mwl 12+yrs plus ila Sina ujasiri wa kupiga mtoto hvyo,naadhibu inapostahiki ,nashirikisha wazazi 100%kwa Kila mtoto ,nawajua wanafunzi wanguu wore nnaowafundisha ukizingua nadeal na wewe kama inavyostahiki ila Sio kupiga kama naua nyoka,mkuu wa Shule akitaka taarifa za mwanafunzi yoyote msumbufu ananiita Mimi kwanza nimueleze then ndo hukumu zinatoka
Hawa watoto wanatoka backgrounds tofauti hatujwa walimu tuwafanyie ukatili,au tulipize tulivyofanyiwa tuko pale kama walezi,wazazi na washauri wao
Sipo kazini Kwa sasa watoto wananimiss juzi mmeenda mmekutana na watoto waeacha Shule Kwa visa TU vya walimu nimeumia mnooo, wanafunzi wananiambia madam ungekuepo ningemaliza Shule Mimi ila daahh mwl Fulani Ndo kasababisha nsimalize Mimi,walimu sisi wengi ni wakatili Mimi nachokipigania mwanafunzi yoyote yule hata awe mvuta bangi ukimtreat fair anakuelewa vzr Sema walimu hatuna saikolojia ya kweli
Wanafunzi wanapigana Mimi nikifika wanaacha,wanafunzi wa form 1 wanaporwa wakija kushtaki naenda Kwa wale wezi wa vidato vya juu huko machimboni nikifika wakiniona utaskia"oohh dogo katuchomesha shika begi Lako bwana hutaniwi"

Nakataa ukatili wa kijinsia Kwa wanafunzi walimua tuache

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Uko sahihi ila soma niliyemjibu hapo ujue hoja gani nimendika
 
so sad
unakuta mwalimu katoka kuachana na mumewe alafu ahsubui anaingia ofisini
whata do you expecting

ila hata kama unastress vipi huwezi kumfanyia hivo mtoto wa mwenzio !!!
 watu kama hawa inatakiwa ndo wawe wa kuwafanyia mfano ili kenge wengine wenye tabia kama hizi wasijitokeze
tena ukiwa na stress na una hekima zako kwa kazi ya ualimu wala huwezi kwenda kazini.
 
Ngoja tuone kama mchukua video atachukuliwa hatua kama yule mteknolojia wa maabara[emoji848]
 
Huyo mbwa bado yuko hai?!, mimi naogopa sana siku nitakuja kuua mtu kwa mambo kama haya, nilishapiga mama wa mtoto wangu hadi akajikolea na kuzimia juu kwa ushenzy kama huu, mola aniepushe kwa kweli, mtoto aadhibiwe kwa mipaka, mpige kwa mkono tu bila silaha yeyote tena miguuni tu na si kwingine
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.

View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

UPDATES: 3

View attachment 2494822

Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Ingekua mwanangu ndio amefanyuwa hivi, huyu mwalimu hata kama serikali imemchukulia hatua bado ningemtengua kiuno walah, singemuacha hivihivi.

Huu ni unyama uliopitiliza
 
Back
Top Bottom