Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Sasa mtoto kama huyo atakuwa amefanya kosa gani mpaka anapewa adhabu kama hiyo kisa kapata 1/10 au
Na pembeni kule wamekaa wengine wanacheka tu kama ni jambo la kawaida linalotendeka [emoji706] kuna watu ni matakataka
Hichi ndio kimenishangaza zaidi, wamekaa wanacheka badala ya kukrmea, hao wote wanapaswa kuchukukiwa hatua
 
Sasa nimeelewa kwanini watoto wanakuwa mashoga tu siku hizi, kama wazazi wenyewe ndo wako hivi. Yaani kuna adhabu ya maana hapo ya mzazi, tena wa kiume, kulalamika tangu jana?!!!!
Mimi ningefika hapo shule kumuongezea mambata huyo mtoto....maana siajabu unaweza kukuta ametenda hata kosa la kumlawiti au kulawitiwa na mtoto mwenzie.
 
Sintoweza kuangalia video inayotia hasira wahuni kama hao adhabu zao zinatakiwa ziwe kubwa sana...ili iwe Fundisho kwa wahuni wengine wakatili kwa Watoto.
 
Mungu anipe uvumilivu wa kutosha sana juu ya washenzi Kama hawa nahisi nitakuja kufungwa mwanangu akifanyiwa hivi ,nitakumaliza kabisa
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.

View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

UPDATES: 3

View attachment 2494822

Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Hawa wawili walio kwenye meza,hata kuwatetea hawa watoto.Nao pia wachukuliwe hatua.Inawezekana ni waalimu pia.
 
Mimi ni mwl 12+yrs plus ila Sina ujasiri wa kupiga mtoto hvyo,naadhibu inapostahiki ,nashirikisha wazazi 100%kwa Kila mtoto ,nawajua wanafunzi wanguu wore nnaowafundisha ukizingua nadeal na wewe kama inavyostahiki ila Sio kupiga kama naua nyoka,mkuu wa Shule akitaka taarifa za mwanafunzi yoyote msumbufu ananiita Mimi kwanza nimueleze then ndo hukumu zinatoka
Hawa watoto wanatoka backgrounds tofauti hatujwa walimu tuwafanyie ukatili,au tulipize tulivyofanyiwa tuko pale kama walezi,wazazi na washauri wao
Sipo kazini Kwa sasa watoto wananimiss juzi mmeenda mmekutana na watoto waeacha Shule Kwa visa TU vya walimu nimeumia mnooo, wanafunzi wananiambia madam ungekuepo ningemaliza Shule Mimi ila daahh mwl Fulani Ndo kasababisha nsimalize Mimi,walimu sisi wengi ni wakatili Mimi nachokipigania mwanafunzi yoyote yule hata awe mvuta bangi ukimtreat fair anakuelewa vzr Sema walimu hatuna saikolojia ya kweli
Wanafunzi wanapigana Mimi nikifika wanaacha,wanafunzi wa form 1 wanaporwa wakija kushtaki naenda Kwa wale wezi wa vidato vya juu huko machimboni nikifika wakiniona utaskia"oohh dogo katuchomesha shika begi Lako bwana hutaniwi"

Nakataa ukatili wa kijinsia Kwa wanafunzi walimua tuache

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mara nyingi walimu wanaopiga watoto hivyo hata kufundisha hawajui. Mwalimu mwenye akili timamu hawezi kumpiga mwanafunzi hivyo
 
-sheria inasema adhabu ya viboko itatolewa pale Panapokuwa na uvunjifu mkubwa sana wa Maadili ya shule, na pia mwalimu anapotoa adhabu ya viboko anatakiwa azingatie ukubwa wa kosa lililofanyika, umri, na jinsia ya mtoto, afya pia ya mtoto, na pia idadi ya viboko vinatakiwa visizidi vinne, na pia Mwalimu wa kiume atamchapa mtoto wa kiume na Mwalimu wa kike atamchapa mtoto wa kike.
- Sina Uhakika kama Sheria inaruhusu Mwalimu kumchapa mwanafunzi kwenye nyayo, ninachojua ni kwenye makalio au mkononi
 
Kumbukeni hata huyo Bwana Mkubwa wa hicho Kijiji siyo msafi kiasi hicho. Aliwachalaza mboko wale Vijana waliotuhumiwa kule Mbeya bila huruma yeyote. Wengi walinyamaza kwa vile allikuwa ni mtoto wa Baba. Je ni nani angeweza kumsema?
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.

View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

UPDATES: 3

View attachment 2494822

Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Kwenye video kuna wapuuzi wanaonekana wanafurahia hilo jambo kabisa

Aisee
 
-sheria inasema adhabu ya viboko itatolewa pale Panapokuwa na uvunjifu mkubwa sana wa Maadili ya shule, na pia mwalimu anapotoa adhabu ya viboko anatakiwa azingatie ukubwa wa kosa lililofanyika, umri, na jinsia ya mtoto, afya pia ya mtoto, na pia idadi ya viboko vinatakiwa visizidi vinne, na pia Mwalimu wa kiume atamchapa mtoto wa kiume na Mwalimu wa kike atamchapa mtoto wa kike.
- Sina Uhakika kama Sheria inaruhusu Mwalimu kumchapa mwanafunzi kwenye nyayo, ninachojua ni kwenye makalio au mkononi
Wataalamu wanatuambia mishipa yote ya damu inapita miguuni na nyayoni. Ndio sababu inashauriwa utembee na kufanya mazoezi kila siku ili kuipa nguvu za kuweza kupitisha damu kiurahisi. Kitendo cha kumchapa mtoto nyayoni kinapaswa kulaaniwa na wote ambao wanaelewa umuhimu wa miguu na nyayo katika maisha ya binadamu. Na ili kutoa haki kwa kitendo cha huyo mwalimu na yeye achapwe idadi Ile ile ya mboko alizomchapa yule dogo tena palepale kwenye nyayo zake wakati miguu yake ikiwa imedhibitiwa kwa staili ileile aliyoitumia.
Nawasilisha.
 
Hawa ndugu zetu walimu sio wote ila baadhi vichwa vyao huwa havipo sawa
Washenzi tu, kipindi nasoma hiyo shule Tulipata Mwalimu wa Kifaransa, Dahhh siwezi msahau alikuwa anafinya na kupiga vibaya, lugha si yangu kunilazimisha juu. Nikatokea kuchukia Kifaransa at very young age kutokana na Mateso.

Hawa walimu wanasoma physiology lakini wanashindwa itumia katika kutoa adhabu na wala kuwaza impact yake academically itakuwaje.
 
haya ndio mambo yanayochangia watoto kukataa shule
Kabisa yaani hii staili ya kuadhibu imenikumbusha akina Adamoo na wenzake kwenye ile kesi ya ugaidi ya Mbowe... Wanatundikwa kama popo juu miguu na mikono imefungwa halafu wanakula mboko kwenye nyayo mpaka zinachanika na mtu anashindwa kabisa kutembea... Yaani hivi mbinu za mateso ya aina hii hata watesi waluobobea huko CIA na FBI Marekani hawatumii kuwatesa magaidi, sisi tunazitumia shuleni halafu other teachers are watching and others are taking video clips...
 
Back
Top Bottom