Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Yanayojiri kwenye Sakata la Mwalimu kumchapa kikatili Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wilayani Kyerwa, Kagera

Kabisa yaani hii staili ya kuadhibu imenikumbusha akina Adamoo na wenzake kwenye ile kesi ya ugaidi ya Mbowe... Wanatundikwa kama popo juu miguu na mikono imefungwa halafu wanakula mboko kwenye nyayo mpaka zinachanika na mtu anashindwa kabisa kutembea... Yaani hivi mbinu za mateso ya aina hii hata watesi waluobobea huko CIA na FBI Marekani hawatumii kuwatesa magaidi, sisi tunazitumia shuleni halafu other teachers are watching and others are taking video clips...
..worse still others are laughing with pleasure ....
 
Tafadhali ni nani anayejua hii shule?

====

UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.

Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.

Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.



View attachment 2494390

UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

UPDATES: 3

View attachment 2494822

Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Dorothy Gwajima wizara imekushinda
 

Attachments

  • IMG_7873.MP4
    17.6 MB
Mimi kilichonishangaza hapo kuona hao wa pembeni wanachekelea kitendo hicho duh nao wapaswa chukuliwa hatua ni watuhumiwa pia
 
Inaitwa shule ya msingi Mbokoo aka stiki
Sijawahi ona mwanafunzi ama mtoto akichapwa unyayoniii
walaka wa adhabu kwa watoto unekataza corporal punishement (bakora) na kama ikotokea ni mwisho fimbo 2 tu. Hivyo hapo amempiga miguuni kwenye nyayo maana yake anajua ni kosa alikuwa na anafanya na anaficha isionekane mtoto kuwa na makovu.
Nmeshikwa na hasira sana kwa hili
 
Kwa sisi tuliosoma shule kama hizo .... Hizo adhabu ni normal sana asee...
Nakumbumbuka watu wasachanwa sana maeneo ya kiuno enzi hizo... Vile uiname mikono uipitishe muiguuni ushike maskio alafu ticha apige stick sita... Ukiiunuka umefuta.
Watu walichanika sana enzi ile..
 
Acheni kukuza mambo, mbona ni adhabu ya kawaida hyo,sijaona cha ajabu hapo labda kama wengi wenu humu mmesomea international school ndo mtashangaa haya
Acha kuandika ujinga humu, huo uchapaji wa kawaida au hiyo clip hujaiona, kausha km vp.
 
-sheria inasema adhabu ya viboko itatolewa pale Panapokuwa na uvunjifu mkubwa sana wa Maadili ya shule, na pia mwalimu anapotoa adhabu ya viboko anatakiwa azingatie ukubwa wa kosa lililofanyika, umri, na jinsia ya mtoto, afya pia ya mtoto, na pia idadi ya viboko vinatakiwa visizidi vinne, na pia Mwalimu wa kiume atamchapa mtoto wa kiume na Mwalimu wa kike atamchapa mtoto wa kike.
- Sina Uhakika kama Sheria inaruhusu Mwalimu kumchapa mwanafunzi kwenye nyayo, ninachojua ni kwenye makalio au mkononi
Na anaeruhisiwa kutoa adhabu ya viboko ni mkuu wa shule tu, mwalimu atatoa adhabu ya viboko pale ataporuhusiwa na mkuu wa shule tu
 
Acha kuandika ujinga humu, huo uchapaji wa kawaida au hiyo clip hujaiona, kausha km vp.
Mbona mnakubal kuchapwa viganjan leo unyayoni ndo imekuwa kesi,tulieni kuna mambo ya msingi ya kudili nayo katika elimu yetu na sio huo upuuzi
 
Hii wiki nimekuwa nazurula kwenye mashule kwa michakato ya kazi zangu .Tunajaribu kuwafahamisha nini cha kufanya na nini wasifanye .Nimekutana na watu wazuri sana ,sijui wanakumbwa na vitu gani lakini wengi niliokutana nao watoto kwa walimu watu safi sana.Tuache ukatili kwa watoto mambo yakigeuka rangi zote utaziona vizuri.
 
Mbona mnakubal kuchapwa viganjan leo unyayoni ndo imekuwa kesi,tulieni kuna mambo ya msingi ya kudili nayo katika elimu yetu na sio huo upuuzi
Kutojadiliwa hayo mambo hakuhalalishi moto kupigwa hivyo, wewe kama huna watoto kausha Mzee mim hata polisi sikupeleki tutamalizana hapohapo shuleni.
 
Kutojadiliwa hayo mambo hakuhalalishi moto kupigwa hivyo, wewe kama huna watoto kausha Mzee mim hata polisi sikupeleki tutamalizana hapohapo shuleni.
Umeshindwa kumalizana na mafisadi,unahangaika na tujitu tudogo
 
Mm siwez nikawa hapo staff nikavumilia icho kinacho tendeka....ova!
Japo sometimes hao watoto wanaweza kukupiga tukio mpka ukapanic.....
Mbona wazungu walisha abolished Stick in their school....
All in all Mungu ni mwema na Mwaminifu wakati wote.....
Umeona watoto wanavyowajibu hovyo na kuwatukana walimu huko ulaya?!
 
Mm siwez nikawa hapo staff nikavumilia icho kinacho tendeka....ova!
Japo sometimes hao watoto wanaweza kukupiga tukio mpka ukapanic.....
Mbona wazungu walisha abolished Stick in their school....
All in all Mungu ni mwema na Mwaminifu wakati wote.....
Tumshukuru aliyerekodi.
Ila nikisikia mwalimu kampiga hivyo mwanangu, eeeeeeh ya Urusi na Ukraine yanahamia Tanzania
 
shule za mikoani zina viboko wale waliosoma miaka ya nyuma kabla internet kuingia mtakuwa mnajua
 
Umeshindwa kumalizana na mafisadi,unahangaika na tujitu tudogo
Kila kitu kwa nafasi yake, chochote kinachozidi ubinadamu lazima kisemwe, mambo ingine ikifatilia sana utajua bara la Africa na baadhi ya mataifa yanayoendelea kuna vitu Bora ubebe jembe ukalime.
 
Back
Top Bottom