Tafadhali ni nani anayejua hii shule?
====
UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.
Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.
Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.
View attachment 2494390
UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.
Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
UPDATES: 3
View attachment 2494822
Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.