Leo ni maadhimisho ya miaka 51 ya sherehe za muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Maadhimisho haya yanafanyika chini ya kauli mbiu inayosema Miaka 51 ya muungano; tudumishe amani na mshikamano, pigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa, shiriki katika uchaguzi mkuu. Hoja yangu ni kwamba; Je ni sahihi kuipigia kampeni katiba inayopendekezwa iliyokosa mtazamo wa kitaifa ktk sherehe za kitaifa kama hizi? Hoja hii inatokana ukweli kuwa upatikanaji wake ulitawaliwa na ubabe wa chama dola, ccm. Au ndo ubabe unaendelezwa!