MAKONDA VYETI VYAKO FEKI""""""""
Kwanza nawasalimu kwa jina la Mungu yeye anayetupa uhai wote tuliopo kwenye hii dunia.
Nimekuwa nafutilia swala linaloendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vyeti vya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda nakutokea maoni mbalimbali.
Wengine wakihitaji aweke vyeti vyake hadharani kuondoa utata uliopo lakini wasemaji wengine wanadai serikali itoke izungumzia swala hilo la vyeti vya Makonda.
Sasa kabla hayo hayajafanyika naomba kueleza machache juu swala hilo.
1. Aliyeibua hoja ya vyeti vya Makonda alishinda tu pale alipoanza kueleza jambo hilo, kwani inaonekana ni jambo la siasa na propaganda sisizo zamsingi nilitegemea siku hiyo angekuja na cheti cha shule ya Msingi cha huyo anadaiwa cheti chake kutumiaka secondary au hata kitambulisho chochote cha mtu huyo kinachoonyesha hilo ndio jina lake halisi na kwamba Makonda amenunua?.
2. Nilitegemea angetokea hata mwanafunzi yeyote aliyesoma na wote wawili na kudhibitisha kuwa anawafahamu na sikweli huyu Mh. Anaitwa hivyo maana naamini wote hao wapo na sitaki kuamini wote watakuwa upande wa Makonda yaani darasa lote wanafunzi wa shule yote wakipindi hicho wawe upande wa Makonda?
3. Nilitegemea hata walimu waliyowafundisha hayo wawili ambao wanawajua kwa majina yao, naamini wengeni wamestafu ila siamini kama walimu wa wanafunzi hayo kama wote wapo upande wa Makonda.
4. Wale wanaosema alete vyeti vyake halali watu wavione je wao wameleta hivyo ambao sio halali hadharani maana hoja hujibiwa kwa hoja Document hujibiwa kwa Document wewe hujaleta Document unataka mwenzio alete wewe unaleta maelezo ukipewa maelezo hutaki hapo tunajifunza nini?
Mnataka tuamini maneno mliyo andika kwenye karatasi nyeupe ?
Hivi serikali iyache kazi ya kuwahudumia wananchi ifanye ya kujibu mambo ya siyokuwa na vieleleza? Mimi nitaamini pale nitakapoona ushahidi wa kutosha na sio uvumi wa kina Mange.
Mh. Makonda endelea kunyamaza maana rais hakukuchagua bila kujiridhisha .
Utazungumza tu kama hayo majibu yangu yatajibiwa hapo juu na sio vinginevyo.