Tetesi: Yanayojiri ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Tetesi: Yanayojiri ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Labda mheshimiwa mkuu kashachunguza na kubaini hili kuwa tuhuma haina ukweli, ndio maana kanyamaza.
Kama tuhuma si za kweli kwanini asithibitisha? Wanavyoacha hili liendelee watu wanazidi kumunguza mmakonda, na wanaoathirika ni familia yake pia.
 
Pole sana
Hahaha
mtaendelea kuwadanganya wapuuzi!!
Uongo hapo ni upi? Kwamba hamna wanaomkataa saul au wanaomuunga mkono ndani ya ccm? Au siyo kweli kwamba bashite ana div 0? Kwako wewe ambae siyo wa kupuuziwa(mpuuzi) kudanganywa kukoje?
 
Kuna jambo dogo tu hapa wenye mamlaka walifanye, watamke ya kuwa Makonda hajafoji au kafoji.
Makonda ni kiongozi wa mkoa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ndani ya mkoa ambao Rais anaishi, sasa anapohusishwa na jambo lolote lenye kuleta utata watu wasilete ushabiki wa vyama.
Kuna sheria ya mitandao iliyopitishwa na ccm na kusainiwa na ccm, kama Makonda ni Makonda hebu sheria hiyo ifanye kazi kwani tuhuma hizi zimeanzia huko na kama Makonda sio Makonda hebu wenye mamlaka wajipime kwenye hili.
Kama ni kweli Makonda sio Makonda basi miaka 5 au 10 sio mingi sana. Wanachosahau ni kuwa ''WATU WANAPITA ILA UTARATIBU UNABAKI'' Sasa mkificha leo akija mwingine baada yenu mtaonekana nanyin mlikuwa HOVYO kana mlivyowaita wa kabla yenu.
Makonda asimame ahesabiwe, serikali hii ilijiwekea utaratibu wa kukanusha hata taarifa ndogo tu sasa hili la Makonda wawaambie watu ukweli.
Makonda ni mkubwa saba kuliko sisi na ana maslahi makubwa sana kwa wanaohoji kwani ni kiongozi tena wa jiji.
 
Kwa style hii nchi itapelekwa kusikojulikana,dereva hajui anaelekea wapi,abiria wakimwelekeza hataki kusikia,hatari sana kwa usalama wetu
 
Kama upumbavu ingekua ni crime, UVCCM wengi wangekua rumande.
 
Uongo hapo ni upi? Kwamba hamna wanaomkataa saul au wanaomuunga mkono ndani ya ccm? Au siyo kweli kwamba bashite ana div 0? Kwako wewe ambae siyo wa kupuuziwa(mpuuzi) kudanganywa kukoje?
Du!! Rudia kusoma utumbo ulio uandika
 
Big brother amejitoa a kilo Kabila katakana seals hili
 
Mbona wengine waliambia waweke vyeti vyao hadharani baada ya tetesi kwamba vyeti vyao vilikuwa na ubabaishaji
 
Porojo bin fedhuli hizo, Lema amewagomea Mbowe, Tundu na Lowasa, walivyomshauri afanye Press conference mbele ya ofici ya Chadema, kuwashukuru viongozi wa cdm, wanachama na wananchi.

Lema kawaumiza kwa kuwaambia kwanza ni lazima akashauruane na mkewe na wanae, na aligoma kupizwa officini kwanza,

Mpasuko CDM unazidi kuendelea
Wewe ni kiazi
 
Taarifa za ndani za CCM ni kwamba mpaka sasa kumetokea mgawanyiko; wapo wanachama na baadhi ya viongozi wa CCM ambao wameunga mkono madai ya wananchi kuzitaka mamlaka zihakiki tuhuma dhidi ya Kada wa CCM na mkuu wa mkoa wa DSM bwana Paul Makonda almaarufu Daudi Bashite, juu ya vyeti vya kitaaluma. Na kundi lingine ambalo linaamini kwamba hata kama mkuu huyo alifeli darasa la saba au hata awe hakufika darasa la saba Kwa maslahi ya c...hama, akingiwe kifua.

Uongozi wa juu wa chama hicho umewaagiza wanachama kutokukuza madai hayo, na badala yake wajiandae Kwa mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwezi huu wa machi, kama maandalizi ya kubadili katiba ya chama hicho, iendane na matakwa ya mwenyekiti wao Mhe. Magufuli. Wasomi mbalimbali na wachambuzi wa masuala ya kiiasa wamedai kuwa CCM inakoelekea, inarudi zama za 'Kudumisha fikra za mwenyekiti'.

Takribani wiki mbili sasa, mkuu wa mkoa wa DSM amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na mijadala mbalimbali, juu ya tuhuma dhidi yake, kwamba anatumia vyeti ambavyo sio vyake, mbali na kufeli kabisa mtihani wa kidato cha NNE Kwa kupata alama Sifuri, pia anasemekana alighushi vyeti.

Ndani ya CCM kinachoendelea ni kulazimishana na kuonyana kwamba wamuache Bashite aendelee na ukuu wa mkoa wasihoji taaluma yake na historia yake ya elimu.
Wasomi mbalimbali kina nani?
 
Back
Top Bottom