Vincenzo Jr
Platinum Member
- Sep 23, 2020
- 24,262
- 58,728
Usiku wa manane
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah, Mkuu umeamua kumvaa Boni Yai leo humuachi apoe ase.Wakuu ngoja mi nilaze tu bichwa langu la kama la Boniyai... muda umeenda
Ule ulikuwa muda wa kujinadi yeye. Ulitaka amsemee nani?Siku ya kujipakulia minyama, kila kitu amaefanya yeye, hado Chadema digital wazo alilipata akiwa prison.
Nafuatilia hapa JF.
Na katika akaunti ya Jambo TV YouTube.
Kote kumewekwa polls na Lissu kaongoza kwa zaidi ya asilimia 85.
Ujumbe huu ni muhimu sana wajumbe wanapaswa kuuelewa.
Uchaguzi gani mpaka hivi sasa haujafanyika ase?
Kwa nini weshindwa kujipanga juu ya jambo hili muhimu.
Hili zoezi wao wenyewe ndio wamelifanya kuwa gumu isivyohitajika. Uongozi ni wazi haukujipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu.Yeah ili kuzuia wapiga kura hewa.
Ni bora zoezi lichukue muda mrefu ila liwe lenye uhakika kuliko kufanya shortcut ambayo ina loopholes
Na kila muda wanatangaza kuongeza wajumbe. Hawa jamaa wananipa mashaka.ni ajabu sana, sasa hivi ni saa 8:06 usiku wa tarehe 22 Januari, 2025 lakini bado tu kura bado hazipigwa!? ni kweli kwamba walijiandaa kwa zoezi hilo?
Wapuuzi tuni ajabu sana, sasa hivi ni saa 8:06 usiku wa tarehe 22 Januari, 2025 lakini bado tu kura bado hazipigwa!? ni kweli kwamba walijiandaa kwa zoezi hilo?
Saba mkuuHapa ili kukamilisha zoezi la upigaji kura kwa hii idadi ya watu 6 kwa mpigo
Itachukua round 166 kukamilisha idadi ya wajumbe wote 996 kupiga kura.
Meanwhile kila round itachukua wastani wa dakika 2 kukamilika. Maana yake hapa kuna masaa yasiyopungua matatu kumamilisha huu mchakato
Na mind you kuna wajumbe kama watatu wameongezwa kwenye list ambao mwanzo hawakuwepo.
166 * 2 /60 = saa 5 na dakika 30.Hapa ili kukamilisha zoezi la upigaji kura kwa hii idadi ya watu 6 kwa mpigo
Itachukua round 166 kukamilisha idadi ya wajumbe wote 996 kupiga kura.
Meanwhile kila round itachukua wastani wa dakika 2 kukamilika. Maana yake hapa kuna masaa yasiyopungua matatu kumamilisha huu mchakato
Na mind you kuna wajumbe kama watatu wameongezwa kwenye list ambao mwanzo hawakuwepo.
Wakuu,
Leo mbali na kuwa ni Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA pia wanasherekea Miaka 32 ya CHADEMA kupata Usajili wa Kudumu, ambapo ulipatikana Januari 21, 1993.
Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?
Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti kwa Bara na Zanzibar, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.
Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?
Orodha ya Wagombea wote ni;
Mwenyekiti Taifa
Makamu Mwenyekiti Bara
- Freeman Mbowe
- Odero Odero
- Tundu Lissu
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
- Ezekia Wenye
- John Heche
- Mathayo Gekul
- Hafidh Saleh
- Said Issa Mohammed
- Said Mzee Said
- Suleiman Makame Issa
Wagombea Wanatoa Salamu kwa Wageni Waalikwa na Wapiga Kura
Tundu Lissu
Lissu amshukuru Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwa kufanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 20, licha ya kutofautiana kimitazamo lakini amekiri hawajawahi kugombana.
"Nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa Chama mfululizo kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatajawahi kugombana, hatujawahi kupigana mimi na yeye binafsi. Ndio tumetofautiana kimsimamo lakini hatujawahi kugombani"
"Vyovyote itakavyokuwa leo, tutakuwa pamoja katika kukijenga chama chetu (Chadema)"
Freeman Mbowe
"Hiki chama tunawajibu wote wa kibinadamu na Wakimungu wakukilinda kwa gharama yoyote ile, na chama hiki hatutakiruhusu kwa gharama yoyote eti kwasababu pengine kura za mbowe hazikutosha au kura za Mhe. Lissu hazikutosha ama za Mhe. Odero yule mzee wetu wa kesho kuna mwanga kwamba kura hazijatosha".
"Uchaguzi huu usiwe vita unapashwa kuwa furaha ya ujenzi wa demokrasia"
"Wako watabiri wengi sana wamesema kuhusu uchaguzi wa CHADEMA, Mhe. Mbowe unaenda kukipasua chama, Mhe. Mbowe inakuaje, hawa ni wanademokrasia, wote kama mnavyowaona. Tofauti zetu kwenye mitazamo hii naamini tunakwenda kuizika mwisho wa kikao hiki tunanelea mbele stronger together"
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ametoa taarifa kwa ufupi kuhusiana na hali halisi ya Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Urais wa mwaka 2020.
Mnyika asoma maazimio ya kamati kuu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa (2024), ambapo yatapelekwa Mkutano Mkuu kwaajili ya kupendekezwa kupitishwa kama maadhimio ya mkutano mkuu wa chama.
Mnyika amehitimisha kwa kuwasilisha mapendekezo ya maazimio ya Mkutano Mkuu
Zoezi la uhakiki wa Wajumbe
Shughuli za uhakiki wa wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zinaendelea katika ukumbi wa Mlimani City.
Uhakiki huo unaongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na kukamilika kwake kutaashiria kuanza kwa uchaguzi wa nafasi za uenyekiti na makamu wa chama hicho Taifa.
Wajumbe 996 wathibitishwa ni halali, zoezi la kura kuanza.
Updates za Matukio
- Mwamakula: Wajumbe wameambiwa kuipiga picha au kuweke alama karatasi ya kura kama ushahidi wa kuongezewa pesa baadaye
- Jumla ya wajumbe wanaoenda kupiga kura ni 996, zoezi la kupiga kura linaanza muda wowote kuanzia sasa
- Frank Mwakajoka kachaguliwa kuwa mwenyekiti wa uchaguzi
- Mgombea Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar: Vijana walipewa nafasi ya kukiongoza chama hawakufanya kitu
Heri waliolala mapema hata wakimka sa9 wanashuhudia mtanange. Hapa natamani nilale kidogo ila nahisi nitapitiwa mazimaHili zoezi litaisha Ijumaa hakika.
Dhana ya uhuru, haki na uwazi ndio inayowapa adhabu.Hili zoezi wamelifanya kuwa gumu wao wenyewe. Uongozi ni wazi haukujipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu.
Bora ulale tu.Heri waliolala mapema hata wakimka sa9 wanashuhudia mtanange. Hapa natamani nilale kidogo ila nahisi nitapitiwa mazima
Hii ngoma inawakuta watu asubuhi wakiwa kwenye foleni kuelekea makazini. Ngoja niweke alarm ya sa 10.Hapa ili kukamilisha zoezi la upigaji kura kwa hii idadi ya watu 6 kwa mpigo
Itachukua round 166 kukamilisha idadi ya wajumbe wote 996 kupiga kura.
Meanwhile kila round itachukua wastani wa dakika 2 kukamilika. Maana yake hapa kuna masaa yasiyopungua matatu kumamilisha huu mchakato
Na mind you kuna wajumbe kama watatu wameongezwa kwenye list ambao mwanzo hawakuwepo.