Sote ni mashuhuda kwamba Freeman Aikaeli Mbowe anaungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu wengi zaidi ya mgombea uenyekiti mwingine yeyote wa chadema, na kwahivyo anakwenda kushinda uchaguzi huu kwa kishindo.
Tayari visingizio kutoka kwa wapambe wa wagombea wanaowafungia wajumbe wao kwenye nyumba za kulala wageni, huku wakikosa kujua ratiba na kinachoendelea kwenye ukumbi wa uchaguzi, wameanza kupiga mayowe ya kushindwa, kanakwamba kuna rafu za uchaguzi hali ya kua wanajitakia wenyewe. Ni vichekesho na makusudi ya kujitakia tu, eti mpaka sasa kuna wajumbe hawajasajiliwa na hawana vitambulisho, wamefungiwa ndani tu.
Prof. Kitila Mkumbo amebainisha wazi kwa umma kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwmba, Freeman Aikaeli Mbowe hawezi kugombea nafasi ya uongozi ambayo hatashinda.
Ni muhimu sana wadau wa JF na wanachadema kwa ujumla, kuzingatia kauli hii ya kitaalamu kutoka kwa mwanafalsafa huyu wa siasa za Tanzania.
Kila la kheri wajumbe,
Kila la kheri Mbowe na Asanti Lisu kwa kushiriki uchaguzi wa chadema ngazi ya taifa.🐒
Mungu Ibariki Tanzania