Yanayosemwa huko Algeria kuhusu tuhuma za kufix mechi ya Tanzania vs Algeria

Kwenye hili kundi, timu iliyostahili kufuzu ni Algeria pekee! Hizo timu 3 zote zilizobakia ni vibonde tu. Angepita Uganda naye angeenda kubebeshwa kapu la magoli tu kwenye hizo fainali, kama itakavyo tokea kwa timu yetu ya Taifa Stars.

Hivyo hata huyo kocha wa Uganda aache kulia lia! Hakuna timu pale. Yule Striker wao Emmanuel Okwi hana tofauti yoyote ile na mzee mwenzake John Bocco.
 
Kiuhalisia kwanza Algeria walibebwa sana. Tanzania tumecheza soka na tumeonesha ukomavu ambao nilikuwa nikitaka uoneshwe siku zote. Hata kama tungefungwa bado timu ya Taifa stars ilijitahidi vya kutosha.
Kwanza goli letu lilikataliwa eti offside
 
Wanasimba punguzeni roho mbaya
 
Kocha wa Niger alisema wataiachia Uganda ili ishinde iende AFCON baada ya mechi yao na Tanzania. Na jana Uganda wakashinda hawakupanga matokeo?
SAYVILLE n
Yaani mkeka wako wa 3+ kuchanika ndiyo unatuletea makelele hapa? Mbona humsemi kwamba Uganda na Niger walipanga matokeo? Nakocha wa Niger alisema kwenye Press Kwa mkapa hapo kwamba watawaachia Kwa madai tulebebwa taifa
Huyu ni mwanasimba,alitaka Kapombe na kenge wenzie wachezeshwe,hivyo timu kufuzu bila hao kenge wake roho inamuuma

Alitamani tutolewe Ili aseme tulijua hawezi kufuzu bila ya wachezaji wa Simba
 
Timu imeshafuzu icheze mastar waumie?

Ikamie mechi waumie?
 
Kama wamechukia basi tubadilishe matokeo.
Tufanye Mahlezi kafunga 1 na Mzize wa Staz nae kafunga 1. Full time 1 : 1 halafu tuone nani kafuzu ndotoni. Nyambafu zao...
 
Wazee wa kubeti mnatema sumu na hasira baada ya kuiua Stars haikufa,huyo Micho anatetea ugali wake.
Kuna Fainali za Kombe la Dunia nadhani mwaka 2002 Senegal alimkanda Ufaransa 1-0. Watu hawakuamini wakabaki kusema wachezaji wa Ufaransa wameuza mechi kwa vile wengi wao wana asili ya Afrika Magharibi. Visingizio hivyo huwa vipo sana kwenye mpira wa miguu hasa timu maarufu na yenye uwezo mkubwa inapopata matokeo mabovu.
 
Mbona yanga iliwafunga wa Algeria kwao.
Upuuzi mtupu , journalist wanamshutumu kocha kwa kupanga matokeo na kocha anamshutumu refa kwa kupanga matokeo.
Mchezo kuhamishiwa uwanja mungine wakwanza kulalamika alikuwa kocha wa Tanzania .
underdog kuleta upunzani sio kitu kipya Kwenye Mpira , Mbona wao algeria walimsumbua Sana Germany Kwenye World Cup ya 2014 au Mbona Morocco aliwafunga vigogo World Cup ya 2022.
Lakini ni masikitiko kuna kundi la watanzania huku Mitaani na Hata mitandaoni hawajaamini kuwa stars iliizuia Algeria aidha walitamani stars ifungwe .
 
SAYVILLE n

Huyu ni mwanasimba,alitaka Kapombe na kenge wenzie wachezeshwe,hivyo timu kufuzu bila hao kenge wake roho inamuuma

Alitamani tutolewe Ili aseme tulijua hawezi kufuzu bila ya wachezaji wa Simba
Wanasimba punguzeni roho mbaya
Mkuu, mbona nimekuwa positive sana kwenye huu uzi aisee? Nionyeshe wapi na lini niliwahi kulilia wachezaji wa Simba waongezwe katika kikosi hiki kilichocheza na Algeria? Tena sana sana nilihoji utegemezi wa wachezaji kama Boko, niambie huyo ni mchezaji wa klabu gani?

Pia ukumbuke uzalendo haupo tu kwa Watanzania. Hata wao kama wameona kuna chengachenga wana haki ya kuhoji kama ambavyo na sisi tungehoji kama hali tusiyoielewa ingetukuta kwa hiyo tusiwashangae kihivyooo. Kuna video ukitaka nitakupostia ya Amrouche, kocha wa Tanzania ambaye ni mualgeria anarushiana maneno na mchezaji wa Algeria baada ya mechi kuisha. Unadhani hiyo inasababishwa na nini?
 
yanga iliyokula sita bil;a ilistahili
 
Sahihi...Kuna chance walituachia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…