Yanayosemwa huko Algeria kuhusu tuhuma za kufix mechi ya Tanzania vs Algeria

Yanayosemwa huko Algeria kuhusu tuhuma za kufix mechi ya Tanzania vs Algeria

Ukweli usemwe Taifa star bila msaada wa third party hatuwezi kuenda Afcon kumbukeni vizuri...
Kwahiyo uganda aliekatuachia ili tufuzu afcon iliyopita nae alifanya nini kwenye hayo mashindano alipoenda?

Dogo umewahi hata kucheza danadana?

Mpira ni hesabu tu na unamatokeo yakikatili mno kuanzia ulaya mpaka huku africa
 
Nimeshangaa yaani aligeria wakose hata goli moko!!🙁 Alafu wako home.!!!?? 🙆
 
Ngoja tutinge robi fainali huko afcon kwenyewe ndo watakuwa na adabu na soka la Tanzania [emoji1241][emoji1241][emoji1241][emoji1241]
 
Ukweli usemwe Taifa star bila msaada wa third party hatuwezi kuenda Afcon kumbukeni vizuri, kipindi kilicho pita hao Waganda ndo walio tuachia mechi na ka fuzi
Tunaenda kupata kichapo kizito
 
SAYVILLE n

Huyu ni mwanasimba,alitaka Kapombe na kenge wenzie wachezeshwe,hivyo timu kufuzu bila hao kenge wake roho inamuuma

Alitamani tutolewe Ili aseme tulijua hawezi kufuzu bila ya wachezaji wa Simba
We Nyumbu wa Serengeti Huko taifa stars wachezaji wa Simba hawakucheza?simba inawachezaji wawili TU Zimbwe na Shomary ?Mzamiru,Kibu ,boko ni wachezaji wa team gani ?
 
We Nyumbu wa Serengeti Huko taifa stars wachezaji wa Simba hawakucheza?simba inawachezaji wawili TU Zimbwe na Shomary ?Mzamiru,Kibu ,boko ni wachezaji wa team gani ?
Aaahaaaa, SAYVILLE kinachomuuma ndo hicho kama ulikuwa hujui

Kama mi nyumbu basi we ni kenge
 
Ukweli usemwe Taifa star bila msaada wa third party hatuwezi kuenda Afcon kumbukeni vizuri, kipindi kilicho pita hao Waganda ndo walio tuachia mechi na ka fuzi

Aise, kumbe Algeria walituachia kabisa tukakosa! Ila Algeria hawakutaka kukaza, kwasababu washapita, ingelikua ni playoff au mshindi wa pili tu, dah tungekula 7. Ila All in All asanteni Algeria kwa kutuachia, kocha wetu pia ni mualgeria Asante sana.
 
Ukweli usemwe Taifa star bila msaada wa third party hatuwezi kuenda Afcon kumbukeni vizuri, kipindi kilicho pita hao Waganda ndo walio tuachia mechi na ka fuzi Afcon kule hatukufanya chochote.
Team ya taifa ni dhaifu ndo ukweli watanzania hawataki kuusikia na hu udhaifu umechangiwa na ushabiki wa timu mbili mnazijua vizuri, pale taifa star nimeangalia mpira sikuona kipaji chochote, Algeria walituachia ile match kiasi kwamba tulipaswa tuofunge kabisa 2-0 ila tulipoteza ata zile chances tulivyo achiwa ndo tukatoka sare.
Agiza pepsi ntalipa.
 
Kuna watu kwenu matokeo mazuri ilikuwa lazima stars ifungwe. Ni Algeria hii yenye USM Algers iliyofungwa pale pale na Yanga aggregate ikawabeba?
 
Mengi yanasemwa kuhusu matokeo ya mechi ya Tanzania vs Algeria iliyoisha kwa suluhu na kuipeleka Tanzania AFCON 2023 huku Uganda ikikosa nafasi hiyo. Nimechukua kama lisaa kufuatilia nini kinasemwa huko nje na nakileta kwenu muone jinsi wanavyotuchafua na kutuona kama hatukuwa na uwezo wa kuwafunga. Naomba niseme kuwa sisemi wala sijawahi kusema Tanzania imenunua hii mechi, hili naomba nilisisitize sana.

Nianze kwa kusema kuwa tuhuma za kufix mechi ni tuhuma nzito sana katika ulimwengu wa soka na siyo tuhuma za kuzichukulia kwa mzaha.

Katika mechi hiyo, Algeria walimiliki mpira kwa asilimia 80, ambazo ni asilimia kubwa sana katika mchezo na pia ukiangalia idadi ya pasi na usahihi wa pasi zao ukilinganisha na sisi ilikuwa ni mbingu na ardhi. Pamoja na hayo Waalgeria wengi wanadhani hiyo ni moja ya mechi mbaya zaidi kwa timu yao katika miaka 5 iliyopita. Wakati sisi tunaona walitawala mchezo, wenyewe wanaona waliboronga mnoo. Nadhani wenzetu wamejiwekea viwango vikubwa mno kwa timu zao.

“It's the 3rd or 4th worst game for the Algerian team since Belmadi's arrival. You could never have guessed that the national team would have such a level. We clearly did not feel that it is a team that occupies the first places in the FIFA rankings.....,” said Yassine Maloumi, a journalist and football specialist.

Algeria Tanzania – “One of the worst matches in Belmadi”

Nadhani wanaodhani hii mechi ilinunuliwa imechangiwa pia na mazingira yaliyozunguka mechi yenyewe. Kwanza kuna maamuzi ya kocha kuamua siku chache kabla ya mechi kutotumia uwanja uliotumika kwa mechi hiyo kwa ajili ya mazoezi ya timu yao. Tukumbuke huu uwanja eneo lake la kuchezea halikuwa kwenye kiwango kizuri na kocha huyo alikuwa anajua hilo na kwa hiyo wachezaji wa Algeria ambao wengi wamezoea kucheza kwenye viwanja vyenye viwango vya juu wangehitaji kufanyia mazoezi pale ili kuuzoea ila kocha wao alibadili mawazo na hakuwapa hiyo fursa.

Algerian team: a new strange decision by Djamel Belmadi causes a scandal

Kabla ya hapo, kuna maamuzi mengine ambayo Belmadi alikuja kujilaumu ya kuipeleka timu kuweka kambi mji tofauti na utakaochezewa mechi jambo ambalo liliongeza usumbufu kwa wachezaji.

A bitter regret for Djamel Belmadi just a few days from Tanzania!

Mtu mmoja alicomment kuwa anadhani kocha wa Algeria alikuwa anataka kumsaidia kocha wa Tanzania ambaye ni Mualgeria mwenzake akigusia kuwa inaonyesha kila wakicheza na timu inayoongozwa na kocha wa kutoka Algeria inaonekana kama wanawafanya feva.

"I noticed every time we play against Algerian manager we do favors , and I think Belmadi was trying to help the new Algerian coach for Tanzania Amrouche"

Kuna wengine wanamtuhumu pia refa alihusika katika kuipendelea Tanzania. Kocha wa Algeria Belmadi alisema refa alikuja kwenye mechi hiyo akiwa na dhamira ya kuibeba Tanzania. Mchezaji wa zamani wa Morocco Abdessalam Ouaddou amemkingia kifua Belmadi kuwa hawezi kuhusika na kufix mechi hiyo ila naye amemtuhumu refa.

“I watched the match and I have to say it’s not true. I know the two coaches and it is not in their values. […] Stop this misinformation. Algeria was weighed down by a referee who clearly came on a mission during qualifying and was certainly appointed for the cause. Algeria fights for integrity and transparency and clean football ,” Ouaddou.

The Algerian team accused of fixing

Kilichobeba uzito zaidi katika tuhuma hizi ni kocha wa Uganda Milutin Sredojević amenukuliwa akisema waziwazi kuwa mechi hiyo imekuwa fixed ili Tanzania iweze kufuzu. Kocha huyu anayejulikana zaidi nchini kama "Micho" amewahi kuifundisha Yanga kwa hiyo tuhuma hizi zinabeba uzito zaidi kutokana na hiyo historia yake. Micho amesema kilichotokea ni aibu kwa mchezo wa soka na ameahidi kufichua zaidi siku za mbele kuhusu tuhuma hizi.

“What happened during the match between the greens and Tanzania is a shame for football… Algeria was complacent with Tanzania and offered them qualification for the Cup from Africa.”

Controversy! Algeria openly accused of having fixed its match against Tanzania

Inawezekana Micho anajaribu kulinda kibarua chake ila tuhuma hizi ni nzito kutoka kwa mtu kama yeye.

Hili jambo nawaachia wakulungwa, mimi kazi yangu imeisha.
Kwahiyo goli la kufunga lilikuwa halionekani!?

Well crafted though..
 
Back
Top Bottom