Yanayotendeka CCM ni uvunjifu wa Katiba na Udikteta, Msajili unayaona?

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Kuna katiba za Aina mbili tu Duniani, Katiba ya Kuandikwa, na Katiba isiyoandikwa. Na kwa Tanzania tunatumia Katiba ya Kuandikwa, Uingereza wanatumia Katiba isiyoandikwa (unwritten). Hakuna nchi au chama chenye katiba zote za aina mbili. Msajiri wa Vyama Nchini anakatiba za maandishi tu za vyama vyote, na nilazima vizifuate.

Nimestushwa sana kwa hiki ninachokiona na kusikia kutoka kwa msemaji wa Chama, kwamba sasa ni marufuku kwa watu kugombea urais na kwamba chama hicho tayari kilishampitisha mgombea wao.

Kama tusipokemea uvunjifu huu wa Katiba ya CCM basi tutakosa sifa ya kupinga uvunjifu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kama Chama tawala kinavunja Katika ya Chama tu, je Katiba ya Tanzania itaheshimiwa na kufuatwa?

Kwasasa Katiba ya ccm haifuatwi katika maongozi ya Chama, kuna kitu kipya kilichotoholewa na Polepole kinaitwa "mila na desturi" ambacho naamini kwa Msajiri wa Vyama vya Siasa hakipo, naamini kule iko Katiba ya CCM. Kikatiba ya CCM inatamka kwamba Rais ataongoza kwa miaka mitano na kisha utaitishwa uchaguzi ndani ya Chama, fomu zitatolewa na Wanachama wenye sifa wataomba kuchaguliwa na chama, rais aliyemaliza muda wa miaka mitano nae anaruhusiwa kuomba kama wanavyofanya wanachama wenzake wa kawaida.

Chama kitamchagua mwanachama mmoja na atachaguliwa kwa kura na kisha atatangazwa kwamba ndie ataingia kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa.. Sasa Humphrey Polepole anazuia na kutisha wanachama wasitumie haki ya kikatiba kugombea, anasema tayari wanamgombea, huyu mgombea kapitishwa lini na chama kipi na kikao kipi?

Msajiri wa Vyama vya siasa ni busara ainuke akemee kama anavyokuwaga mwepesi kwa vyama vingine kuona kama katiba ya ccm inafuatwa.
Wako watu wachache ambao ni wajinga wa kuzaliwa, wanasema kwanini naijadili ccm mimi mwanachadema, Hawa ni wajinga hawajui makosa ya ccm yanaathiri Taifa zima bila kujali chama. Ubovu wa ccm leo umesababisha nahangaika kupata sukari nk. Hivyo kwa dhana hiyo na nyingine nyone ccm inanihusu na inamhusu kila Mtanzania kwa 💯. Ikitaka tusiijadili itoke madarakani, isihusikw na maisha yetu.
 
Attachments

  • 101603652_105951134407490_8870718768643938615_n.mp4
    12 MB
Yericko,

Ukitaka kuua nyoka anzia miguuni mwako..!!

Wanachama na viongozi ndani ya Chadema wamefukuzwa bila kupewa haki ya msingi ya kusikilizwa kama katiba inavyoelekeza,, lakn mmekaa kimya.

Ruzuku na michango vinatafunwa kama karanga na Chairman huko Chadema pasipo kufuata taratibu,, lakn mmekaa kimya

Chama nyakati za kampeni kinakopeshwa mikopo ya riba na Mr Chairman, wkt huo huo ruzuku na michango vinatumika kulipia hilo deni kwa chairman pasipo kufanyiwa uhakiki,, lakn mmekaa kimya

Tuanze na ya nyumbani kwanza kabla ya kutoa jicho kwa jirani, unless kama kwa jirani panavutia sana basi tuhamie huko!!!!!!
 
kabisa yaani nafasi ya Urais inakwenda kwa mazoea kuwa kusiwepo mtia nia kama Bernard Membe
Mzee Bernard Membe baada ya kujitathmini 2015 na pia kuonesha nia ya kuomba apitishwe kugombea nafasi ya Urais 2020 je ataruhusiwa kupata walau nafasi ya kujieleza mbele ya vikao vya CCM ili wamfikirie?

Mwaka 2015 mwezi Juni kutoka ktk maktaba online

Maneno mazito ya Mzee Bernard C. Membe bado yanaishi mpaka leo kwa wanaCCM ambao wanaitakia mambo makubwa zaidi nchi hii wakielekea 2020, tumsikilize :
 
Huku Mwenyekiti John Pombe Joseph Magufuli akiwaasa aliowaita diehards wenye maslahi yao binafsi kama kina the Polepoles (siyo Humphrey Polepole) wasiwazibie wanachama wa CCM haki ya kutia nia kwa kwa kisingizio cha 'Mila na Desturi' kisha kutoa nafasi ya makundi inayoweza kuleta mpasuko wa kisiasa ktk CCM Mpya
 
Kikatiba ya CCM inatamka kwamba Rais ataongoza kwa miaka mitano na kisha utaitishwa uchaguzi ndani ya Chama, fomu zitatolewa na Wanachama wenye sifa wataomba kuchaguliwa na chama, rais aliyemaliza muda wa miaka mitano nae anaruhusiwa kuomba kama wanavyofanya wanachama wenzake wa kawaida.

Chama kitamchagua mwanachama mmoja na atachaguliwa kwa kura na kisha atatangazwa kwamba ndie ataingia kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa...

Kiongozi hii katiba yangu ya 2010 nahisi imechakachuliwa, hicho kifungu sikioni, naomba unisaidie namba ya kifungu nirejee.
Nilichoona ni kwamba ikifika kipindi cha uchaguzi Halmashauri kuu itapendekeza majina “Yasiyozidi” matatu na kuyapeleka kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kuchagua mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM.
 
Siamini kwamba katika karne hii, watu aina hii bado wapo duniani! Kama kweli hawa ndio viongozi wa chama tawala nchini Tanzania...basi hadithi yangu inaishia hapo!
 
Tusitishane bwana! Unajuwa wewe yeriko nyerere. Hiyo unayoongea nayo ni spika tu
Ukiona spika inatoa sauti kubwa ujuwe kuna MTU yupo nyuma ya mic anachagua tu spika zenye watts kubwa anaipachika waya nyuma ili asikike
 
Yericko,

Ukitaka kuua nyoka anzia miguuni mwako..!!

Wanachama na viongozi ndani ya Chadema wamefukuzwa bila kupewa haki ya msingi ya kusikilizwa kama katiba inavyoelekeza,, lakn mmekaa kimya.

Ruzuku na michango vinatafunwa kama karanga na Chairman huko Chadema pasipo kufuata taratibu,, lakn mmekaa kimya

Chama nyakati za kampeni kinakopeshwa mikopo ya riba na Mr Chairman, wkt huo huo ruzuku na michango vinatumika kulipia hilo deni kwa chairman pasipo kufanyiwa uhakiki,, lakn mmekaa kimya

Tuanze na ya nyumbani kwanza kabla ya kutoa jicho kwa jirani, unless kama kwa jirani panavutia sana basi tuhamie huko!!!!!!
Yericho mwenyewe kila akiweka jina anatolewa baru
 
Desturi ya ccm ndio sheria zenyewe mangi
Huku Mwenyekiti John Pombe Joseph Magufuli akiwaasa aliowaita diehards wenye maslahi yao binafsi kama kina the Polepoles (siyo Humphrey Polepole) wasiwazibie wanachama wa CCM haki ya kutia nia kwa kwa kisingizio cha 'Mila na Desturi' kisha kutoa nafasi ya makundi inayoweza kuleta mpasuko wa kisiasa ktk CCM Mpya
 
Kiongozi hii katiba yangu ya 2010 nahisi imechakachuliwa, hicho kifungu sikioni, naomba unisaidie namba ya kifungu nirejee.
Nilichoona ni kwamba ikifika kipindi cha uchaguzi Halmashauri kuu itapendekeza majina “Yasiyozidi” matatu na kuyapeleka kwenye mkutano mkuu kwa ajili ya kuchagua mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM.
Mwambie akupe katiba ya chadema kwanza
 
Back
Top Bottom