Kuna katiba za Aina mbili tu Duniani, Katiba ya Kuandikwa, na Katiba isiyoandikwa. Na kwa Tanzania tunatumia Katiba ya Kuandikwa, Uingereza wanatumia Katiba isiyoandikwa (unwritten). Hakuna nchi au chama chenye katiba zote za aina mbili. Msajiri wa Vyama Nchini anakatiba za maandishi tu za vyama vyote, na nilazima vizifuate.
Nimestushwa sana kwa hiki ninachokiona na kusikia kutoka kwa msemaji wa Chama, kwamba sasa ni marufuku kwa watu kugombea urais na kwamba chama hicho tayari kilishampitisha mgombea wao.
Kama tusipokemea uvunjifu huu wa Katiba ya CCM basi tutakosa sifa ya kupinga uvunjifu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kama Chama tawala kinavunja Katika ya Chama tu, je Katiba ya Tanzania itaheshimiwa na kufuatwa?
Kwasasa Katiba ya ccm haifuatwi katika maongozi ya Chama, kuna kitu kipya kilichotoholewa na Polepole kinaitwa "mila na desturi" ambacho naamini kwa Msajiri wa Vyama vya Siasa hakipo, naamini kule iko Katiba ya CCM. Kikatiba ya CCM inatamka kwamba Rais ataongoza kwa miaka mitano na kisha utaitishwa uchaguzi ndani ya Chama, fomu zitatolewa na Wanachama wenye sifa wataomba kuchaguliwa na chama, rais aliyemaliza muda wa miaka mitano nae anaruhusiwa kuomba kama wanavyofanya wanachama wenzake wa kawaida.
Chama kitamchagua mwanachama mmoja na atachaguliwa kwa kura na kisha atatangazwa kwamba ndie ataingia kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa.. Sasa
Humphrey Polepole anazuia na kutisha wanachama wasitumie haki ya kikatiba kugombea, anasema tayari wanamgombea, huyu mgombea kapitishwa lini na chama kipi na kikao kipi?
Msajiri wa Vyama vya siasa ni busara ainuke akemee kama anavyokuwaga mwepesi kwa vyama vingine kuona kama katiba ya ccm inafuatwa.
Wako watu wachache ambao ni wajinga wa kuzaliwa, wanasema kwanini naijadili ccm mimi mwanachadema, Hawa ni wajinga hawajui makosa ya ccm yanaathiri Taifa zima bila kujali chama. Ubovu wa ccm leo umesababisha nahangaika kupata sukari nk. Hivyo kwa dhana hiyo na nyingine nyone ccm inanihusu na inamhusu kila Mtanzania kwa [emoji817]. Ikitaka tusiijadili itoke madarakani, isihusikw na maisha yetu.