Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
Kinachotokea Kenya sasa baadhi wa Watanzania wanawasifu raia wa Kenya Kuwa wameelimika zaidi kudai haki zao kuliko wa Tanzania.
Wanaosema hivyo labda wamezaliwa miaka ya 1999 kuja 2000.
Tanzania 🇹🇿 walifanya haya wanayofanya Kenya 🇰🇪 miaka 23 iliyopita .
Yaani Mwaka 2001 Chama Cha Wananchi C.U.F waliliamsha dude ambalo kwa historia ya Tanzania haliwezi kusahaulika kwani kwa Mara ya kwanza Watanzania walikua wakimbizi baadhi walikimbilia Shimoni Mombasa Kenya 🇰🇪 na wengine walikimbilia Somalia..yaani Somalia hii tunayoijua ilikua na wakimbizi kutoka Tanzania 🇹🇿 na baadhi inasemekana hawajawahi kurudi .
Vurugu hizo wakati huo CUF ilikua na nguvu mno ilisababisha zaidi ya watu 1000 kufariki Dunia. Wafuasi wa C.U.F walikua wakilalamika matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2000 Kuwa mgombea wao alishinda dhidi ya mgombea wa CCM (Benjamin Mkapa) Ila matokeo yamepikwa na kumtangaza mgombea wa CCM, malalamiko meengine walikua wakikosoa Serikali ya Mkapa kubinafsisha mashirika ya Umma ambayo yaliwaacha Watanzania wengi bila ajira ,miongoni mwa vitu vilivyoninafsishwa ni Kiwanda Cha kutengeneza matairi ya Magari Cha General Tyre kilichokua maarufu zaidi Afrika kwa tairi zilizobora zaidi Ambapo alieshinda zabuni ya ununuzi wa kiwanda hicho alikua Mkenya ambaye baada ya kununua alikifunga kiwanda kwa madai Mashine zilikua Chakavu na kuwaondoa wafanyakazi wote na kuwaacha bila ajira na inasemekana Mashine zile alizihamishia Kenya na kufungua kiwanda Cha Yana Tyre.
C.U.F waliliamsha mno enzi zao wakiwa na kauli mbiu yao 'Ngangari au jino kwa jino mikoa ya pwani ndio walikua na wafuasi wengi zaidi mikoa Kama Dar,Lindi,Tanga,Mtwara,Morogoro na Pwani .
Kwenye kitabu Cha Mkapa ameelezea zaidi Mambo hayo na kusema moja ya dosari katika Utawala wake ni sheria ya ubinafsishaji mashirika ya Umma iliyokua na dosari nyingi na vurugu za mwaka 2001.
Hali ile ilimfanya msanii Juma Kiroboro (Sir Nature ) kuingia studio na Prof Jay kutunga wimbo..