Yanga acheni kuhangaika na Feisal, ni ushamba

Yanga acheni kuhangaika na Feisal, ni ushamba

Sakata la Feisal na Yanga linaendelea kupamba moto. Bahati mbaya hizi timu za Simba na Yanga zina maujinga sana. Ndio maana utaona kila siku zinakuwaga na habari za wachezaji waliowakariri. Utasikia Manzoki, Miquisone kila timu inawataka. Hamnaga scouting timu za maana?

Hivi sasa nasikia Yanga hawataki Feisal aondoke. Yani akae aendelee kulipwa pesa ya mboga wakati kapata mkataba wenye maslahi mazuri? Yani hivi leo huyo mchezaji akifariki hiyo timu itakufa pia?

Badilikeni. Mchezaji kapata mahali pengine nilitarajia mumjenge kiasikolojia hata game ya kesho acheze kwenu tena mseme mnaitumia kumuaga.

Ingieni sokoni mbona bara la Afrika lina vipaji vingi sana?

Wachezaji nowadays wameanza kuelewa kuwa soka ni ajira sio yale maupuuzi walioyofanya kina Boban, Ngasa, nk. Alafu mtu akistafu akiugua hata pesa ya matibabu hana, anaanza kuomba msaada.

Yanga acheni ushamba, mwacheni Feisal aende. Uonesheni professionalism katika sakata hili.

Naongea kama shabiki wa Yanga ninayependa mafanikio ya Yanga na mafanikio binafsi ya wachezaji.

Fei Toto katufanyia mengi, katumia haki yake. Hakuna sababu yoyote ya kutaka kumvuruga. Anaweza kwenda na akarudi tu ikiwa atatoka kwa mawasiliano mazuri

Na mimi nakushauri Feisal, wakikulazimisha baki alafu ukiingia uwanjani cheza chini ya kiwango. Au cheza rafu za wazi uwe unapigwa red card tu kila mara. Watakuacha wenyewe.


Tubadilike
Mkuu, ni haki ipi hasa unayoipigania hapa? Unaelewa nini kuhusu mkataba? Tuache kuandika mada za kusherehesha majukwaa tuje na logical reasoning
 
Faisal kaishia darasa la saba B anatetemesha nchi,mimi na masters yangu dina hata kibarua
Mjinga mmoja kwenye dabate alidai efucation is better than money
 
Kama Feisal amefuata mkataba kwa kununua sehemu iliyobaki basi Yanga waombe huruma tu ya Feisal, lakini sababu walizotoa za kutaka mkataba uheshimiwe hazina mashiko, kwani Feisal kuvunja mkataba kwa kununua sehemu iliyobaki hajakosea popote, wao Yanga SC ndio wanatakiwa kuheshimu mkataba.

Hili suala linaonesha vile vilabu vikubwa huweka vipengele kwenye mikataba ya wachezaji wao hasa wa ndani kwa mazoea, wakidhani hawawezi kuondoka kwa sababu ya mapenzi, wabadilike iko siku watalia.
Tatizo la Vilabu vyetu ni Uswahili

Tatizo la Wachezaji wa Kitanzania ni misrepresentation, kuna wachezaji wanajiwakilisha wenyewe na shule hawakwenda.

Mchezaji anakuwa na wakala shabiki wa timu anayoenda cheza

Ili wachezaji wa Kitanzania wafaidi matunda ya vipaji vyao, yawapasa kutafuta mawakala wazuri,
Yawapasa kuacha kuwa washabiki wa timu
Yawapaswa kuwa professional

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom