Yanga acheni tabia za kuwaza ushirikina kila mnapobanwa mbavu!

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
7,051
Reaction score
12,566
Leo nimeshangaa sana Kaseke na mwenzake kwenda goli la mpinzani kuanza kutikisa nyavu kama wanatafuta kitu hivi kwa chini,baadaye wakaenda hadi kwenye taulo la golikipa na kulikung'uta!Nilipigwa na butwaa kuona hivyo!Wakati huo Matokeo yakiwa Prison 1-0 Yanga na Yanga walikuwa wakishambulia sana!
Hii tabia si nzuri hasa kwa timu inayoshiriki ligi kuu na Club kubwa kama Yanga!Mnatia aibu kwakweli na hii sio mara ya kwanza ninyi kufanya hivyo!
Prison mnalingana nguvu maana kwenye mechi ya kwanza mlitoka sare tena kwenu!Sasa mnachoshangaa ni nini wao kuongoza kwa goli moja na ninyi mkiwa mnakosakosa?
Aibu kwenye michezo,mechi zinaonekana mpaka nje ya nchi halafu mnafanya ujinga!Shwain kabisa!

Siku nyingine mkagoma kuingilia lango la kuingia uwanjani,ninyi watu gani?Mbona mnaupa sana promo ushirikina?

Nawatakia kheri ya mwaka mpya!
 
Teh teh teh 😁😂👍 ngoja wazee wa kubeba ubingwa wa VPL ndani ya round ya kwanza tu waje wakutolee povu.

Eti ubingwa ni wetu awamu hii? Kumzidi Simba points 2 ikawa tayari wamekuwa mabingwa. Sijui ni stress ndo zinawafanya wawaze hivyo?
 
Simba akifanikiwa kula viporo vyake basi watakuwa sawa kwa point!Nadhani hilo ndio liliwapa pressure mpaka wakawaza ushirikina!
 
Ni nadra sana hii klabu kumaliza msimu bila kuonesha imani za kishirikina. Hata viongozi wao wanaimani hizo hizo ndio maana wachezaji wao hawakemewi. Ila ni kitendo cha aibu kwa klabu kubwa kama hiyo na dunia ya sasa kuwa na mchezaji anaeamini kuwa goli halijafungwa sababu ya kulogwa.
 
In short yanga wameonyesha negative attitude, hayo mambo sio ya kifanywa na professional players
Klabu kubwa kama Yanga wanaruhusu wachezaji wao kufanya upuuzi wa kiwango hicho?Uongozi wa Yanga unapaswa kuwakemea wachezaji wao,waoneshe kiwango ili washinde na sio failure zao wanatafuta mchawi!
 
Ni nadra sana hii klabu kumaliza msimu bila kuonesha imani za kishirikina. Hata viongozi wao wanaimani hizo hizo ndio maana wachezaji wao hawakemewi. Ila ni kitendo cha aibu kwa klabu kubwa kama hiyo na dunia ya sasa kuwa na mchezaji anaeamini kuwa goli halijafungwa sababu ya kulogwa.
Its a shame!
 
Umejuaje kuwa kufanya hivyo ni ushirikina
 
Klabu kubwa kama Yanga wanaruhusu wachezaji wao kufanya upuuzi wa kiwango hicho?Uongozi wa Yanga unapaswa kuwakemea wachezaji wao,waoneshe kiwango ili washinde na sio failure zao wanatafuta mchawi!
Mbona unalazimisha hili Jambo lionekane kubwa kiasi hicho?Hivi kwa nchi yetu hii ni timu gani haijawahi kufanya au kwenda kwa mganga kwa ajili ya Mambo haya ya kishirikina?
 
Mkuu itakuwa wewe ni mshirikina. Kwa nn utoe hitimisho kuwa kwa kitendo hicho cha wachezaji wa Yanga kutikisa nyavu wanaamini ushirikina.
 
Mbona unalazimisha hili Jambo lionekane kubwa kiasi hicho?Hivi kwa nchi yetu hii ni timu gani haijawahi kufanya au kwenda kwa mganga kwa ajili ya Mambo haya ya kishirikina?
Level hizo za kishirikina hamjavuka bado?Ushirikina hauna nafasi kwenye soka la kisasa lasivyo Nigeria,Congo wangekuwa wameshachukua world cup!
Badilikeni!
 
Kitu kafanya kaseke, sasa unahusishaje Yanga yote?
Sio kaseke peke yake,pamoja na mchezaji mwingine!Walikuwa wawili!Halafu timu nzima ilishawahi kutopitia lango la kuingilia kwa imani hizo hizo!
Uongozi wa Yanga unapaswa kukemea hilo!
 
Back
Top Bottom