Yanga Afrika inabebwa

nandengele

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
689
Reaction score
805
Katika kuangalia kwangu mechi mbili za Yanga kwenye michuano ya mapinduzi cup naona dhahiri shairi kuna upendeleo kwenye timu ya Yanga.

Hili ni tatizo na nasema kabisa haitaweza kufanya vizuri kwenye mashindano ya Africa
 
Last edited by a moderator:
Azam litimu halina nidhamu wala halichezi football bali rugby. Hovyo kabisa
 
Kama ni goli la yanga ni goli halali kabisa halina utata wowote
 
Hakika mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni kwakigezo gani ambacho unaona Yanga wanabebwa?
 
Katika kuangalia kwangu mechi mbili za Yanga kwenye michuano ya mapinduzi cup naona dhahiri shairi kuna upendeleo kwenye timu ya yanga.Hili ni tatizo na nasema kabisa haitaweza kufanya vizuri kwenye mashindano ya Africa
Sawa unao uhuru wa kuongea
 
Hakika mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni kwakigezo gani ambacho unaona Yanga wanabebwa?
Tuwe wa kweli angalia maamuzi mengi ya refa yalikuwa ni ya kuingamiza Azam,tukianzia kwenye fouls yanga walistahili kupata kadi mbili nyekundu kwa wachezaji Abdul na donald ngoma lakin refa akaacha sasa kama sio kubebwa nn, marefa wetu hawako fair hata kidogo, napenda kuwaambia hamtafika mbali kwenye CAF orange champion
 
Ni kweli kitendo alichokifanya D.ngoma kumsukuma mdahil sio cha kimichezo alistahili kuashibiwa ata kw kadi ya njano lkn hakuna..Yondani kamtemea mate Boko lkn hakuna kadi..juma Abdul pia alifanya rafu mbaya pia hakuazibiwa..eti mechi ya kibabe vle hakuna kadi kw yanga..
 
Hamna kitu, tatizo Azam walikuwa wanacheza na refa,
Wamebadilika sana kimpira sio azam ile tuliyoijua, ni kama wana stress vile, fujo nyingi hakuna mpira ule wa kugonga ambao wao ndio walikuwa wanacheza zamani, angalia takwimu za mchezo, mapumziko had mwisho wa mchezo zilikuwa zinaibeba yanga
 
Kitimu Yanga ipo vizuri,ila kwa namna moja ama nyingine refa ameharbu sana mechi ya leo kwa kuachia makosa mengi ya utovu wa nidhamu uwanjani
 
unajisumbua bure na vitusi vyako et unawatukana wazazi wangu unafikir unaniumiza, mara nyingi unapo posti kitu kwenye social media tegemea mema na matusi sasa kwa nini niumie
 
Una mtaka maneno Jerry Muro, mmekomaa ili apotee kwenye tasnia ya michezo, haya we.
 
Tukiachilia mbali ushabiki wa vilabu vyetu,nilichoweza kukiona kwenye mechi ya Jana ni kiwango kikubwa cha utovu wa nidhamu kutoka timu zote mbili.

Hii nikuanzia wachezaji mpaka viongozi,nidhamu mbovu ikaufanya mchezo kua wa hovyo na timu kushindwa kuonesha viwango vyao stahiki.

Sina haja ya kuwazungumzia waamuzi kwani suala la waamuzi wetu limekua ni tatizo sugu,nilazima tukubali kua hatuna waamuzi wenye viwango bora.

Mambo yote haya yanachagizwa na vyama vyote vinavyoshughulika na mchezo huu wa mpira wa miguu vikiongozwa na baba wao TFF.Tunasafari ndefu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…