Ile Mechi ya 1989 usiifananishe na Mechi nyingine. Hakuna cha maana kilifanyika na kina Makelele zaidi ya Yanga kutimiza maelekezo ya FAT. Nchi hii Hakuna ushabiki bila Simba na Yanga kuwa kwenye ligi moja. Kuna watu huwa nawasikia wanajifariji eti ili soka likue Simba na Yanga zife Kwanza. Hawajui historia. Yanga alipoteteleka na kuzaliwa Pan African imara Hakuna cha maana kilichotokea, na Simba ilipoteteleka Hadi kukaribia kushuka daraja, Yanga walilazimika kugharimia ubingwa uliobebwa na Coastal Union ili mtani wao asishuke daraja.
Wakati huo Pamba ilikuwa Moto na ilikuwa kama Tawi la Simba. Lakini isinheweza kuchukua nafasi ya Simba.