Yanga bado hakuna professionalism

Yanga bado hakuna professionalism

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Morrison bado yupo kwao.

Aziz Ki bado yupo kwao.

Feisal tunaambiwa hana professional kutoka kambini sawa

Lakini Hawa Azziz key na Morrison wanajua kesho yanga ana game ngumu na IHEFU ambayo alipoteza game iliyopita wachezaji

Morrison
Aziz
Feisal
Bangala wote hawapo halafu tukikosa matokeo tunaanza kutafuta mchawi.

Bado yanga hatuna professional hatupo serious bado watu wanalipwa pesa kibao za bure morrison analipwa mil 18 kwa mwezi ili akae kwao?

Viongozi acheni utoto Hawa watu waitwe kambini haraka Sana!!
 
Yanga wanashangaza sana

Wako radhi wawalipe wageni 20M ila feisal anayewafungia kila match wampe 3M

Binafsi natamani dogo apate team ya maana hata kama ni mkataba avunje awalipe

Mpira una umri asijezeeka na jina kubwa bila mali
 
Yanga wanashangaza sana

Wako radhi wawalipe wageni 20M ila feisal anayewafungia kila match wampe 3M..
Tusiendeshwe kwa hisia kiasi hicho. Kazi yoyote ni mapatano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Hakuleweshwa pombe, hakurukwa na akili na wala hakushikishwa bunduki kusaini mkataba wakati ameuona hauna maslahi kwake.

Ni serikalini peke yake ndio wanaolipana mishahara kwa kufata rank. Ila kwa taasisi binafsi ni swala la mapatano. Ni kawaida kuona dereva X analipwa sh laki tano kwa mwezi wakati dereva Y analipwa laki nane tena pengine hata elimu kazidiwa na X. Sasa usiingiwe na wivu kisa mwenzio analipwa zaidi, kama huoni maslahi kwako usikubali kuingia kandarasi ya kuifanya kazi, tafuta pengine. Ni rahisi tu
 
Tusiendeshwe kwa hisia kiasi hicho. Kazi yoyote ni mapatano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Hakuleweshwa pombe, hakurukwa na akili na wala hakushikishwa bunduki kusaini mkataba wakati ameuona hauna maslahi kwake. Ni serikalini peke yake ndio wanaolipana mishahara kwa kufata rank. Ila kwa taasisi binafsi ni swala la mapatano. Ni kawaida kuona dereva X analipwa sh laki tano kwa mwezi wakati dereva Y analipwa laki nane tena pengine hata elimu kazidiwa na X. Sasa usiingiwe na wivu kisa mwenzio analipwa zaidi, kama huoni maslahi kwako usikubali kuingia kandarasi ya kuifanya kazi, tafuta pengine. Ni rahisi tu

Sio kesi
Akipata wa kumlipa vizuri aendeee
 
Sawa sio kesi
Ila akipata pakueleweka aendee
Yaah ila inabidi afuate utaratibu ndio mpira upo hivyo, Saidio Mane aliwaambia Liverpool wamuongezee mzigo, Liverpool wakagoma.Mane hakugomea mazoezi wala mechi ila aliwakatalia kusaini mkataba mpya sababu hawakutaka kumuongezea mzigo.

Mkataba wake ukaisha mwaka jana kaondoka FREE Bayern na Bayern wanampa mzigo mkubwa kuliko Liverpool. Hiyo sasa ndio tunasema mzezaji huyu ni proffesional na si huyo aliyegoma ambaye najua mwisho wa siku yy ndiye atakaeumia na si Yanga.
 
Njia ya kupambana na aina ya wachezaji wasio watiifu ni kuwekeza kwa vijana kama kina mzinze na kuamini process nje ya hapo itaendelea kuwa tabu
Kama hao uliowataja wako kwao sioni umuhimu wa kuendelea kuwa nao pale mkataba utakapomalizika
 
Yanga wanashangaza sana

Wako radhi wawalipe wageni 20M ila feisal anayewafungia kila match wampe 3M

Binafsi natamani dogo apate team ya maana hata kama ni mkataba avunje awalipe

Mpira una umri asijezeeka na jina kubwa bila mali
Cha home hakinaga thamani!
 
Mmeanza kupopoana? sisi bado hatujamaliza kutangaza wachezaji zimebakia dakika kadhaa tutetemeshe nchi
 
Yanga wanashangaza sana

Wako radhi wawalipe wageni 20M ila feisal anayewafungia kila match wampe 3M

Binafsi natamani dogo apate team ya maana hata kama ni mkataba avunje awalipe

Mpira una umri asijezeeka na jina kubwa bila mali
Kwa mfano wako huu, basi hata walimu waanze kulipwa mishahara na posho nono kama zile za wabunge.

Maana wanafanya kazi kubwa ya kuzalisha wasomi, na pia katika mazingira magumu, ukilinganisha na wabunge ambao kazi yao kubwa ni kugonga tu meza na kuitikia 'ndiyooooooo'!!

NB: mshahara kwa mchezaji unatokana na yeye mwenyewe kukaa mezani na mwajiri wake, halafu wanafanya makubaliano.

Duniani kote mishahara ya wachezaji huwa hailingani. Kila mchezaji hulipwa mshahara kutokana na mkataba wake alioingia na club. Hakuna njia ya mkato kama hiyo ya Fei Toto.
 
Back
Top Bottom