Yanga bado wana kitu cha kujifunza kimataifa kutoka kwa Simba, Mnachofanya wana Yanga ni sawa na Newcastle kukebehi Man U kufuzu UCL

Simba sio mbovu shida tu ni kujilinganisha na yanga
 
Itakuwa ni mwenda wazimu wa kiasi cha juu kujifunza kwa simba hii tia maji tia maji
 
Unafurahisha wewe msimu wa 2021/2022 Simba mlipowanga kule Afrika Kusini, mlifungwa na ASEC MIMOSAS tatu bila. ASEC MIMOSAS hawakuchezea uwanja wao halisi Ivory coast, bali walichezea Niger. Mtatafuta kila sababu ila timu yenu ya Simba Kwa sasa Haina kiwango kizuri. Mjitahidi mpambane Super League msiche kutia aibu Taifa.
 
Aahaaaaa,wanahama Kila kichaka
 
Nani kibonde hapa
Iyo timu iliyotoka shirikisho ina shiriki kombe gani msimu huu? Nyie mlicheza na vibonde hilo usipinge kufika fainalii sio hoja ya kujifunza kwa yanga hata machizi one time wanapataga akili
 
Mwakarobo katika ubora wake.
Simba ni mbovu sanaaa.
Full stop
 
Hongereni sana watani kwa kuvunja mwiko wa miaka 25 na kutinga makundi ya Klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998. Ni jambo kubwa sana kwa wana Uto wote. Mnastahili pongezi. Japo mmeingia kwa kuwatoa wakimbizi lakini si mbaya.

Sisi tumezoea kuingia makundi kwa miaka mingi. Ni vitu vya kawaida kwetu. Lakini kwenu huu ni muujiza. Kidogo mlikua mnaliwezea lile kombe la "Loser" lakini huku kwenye klabu bingwa mlikuwa mnatepeta mapema sana. Mmekua "sokomoko" kwa miaka 25. Hatimaye leo mmevunja mwiko. Japo sijui ni upi maana mnapenda kusema "mbele mwiko nyuma mwiko" lakini nachojua mwiko mmoja umevunjika leo baada ya miaka 25. Hongereni sana.

Mara ya mwisho kufika makundi klabu bingwa ni 1998 wakati Mayele akiwa na miaka minne, Feitoto alikua mimba, na Whozu alikuwa na mwaka mmoja lakini leo anaitwa Chibaba [emoji1787]. Makundi pekee mliyokua mnaingia mara kwa mara ni ya Whatsapp. Kwahiyo hongereni sana kwa kuvunja mwiko.

Ilikua inatia simanzi sana wakati Simba tukienda group stage, nyie mnarudi kuosha vyombo na Njombe Mji au Itilima FC. Lakini mwaka huu ni furaha kwamba kaka zenu tumepata watu wa kutusindikiza kwenye makundi ya klabu bingwa. Raha mliyoipata leo, sisi tumeipata mfululizo kwa miaka mingi.

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Uto, hasa wenye umri chini ya miaka 25 hawajawahi kuishuhudia klabu yao ikicheza makundi klabu bingwa. Na walikua na hatari ya kuzeeka bila kuiona timu yao ikitinga hatua ya makundi. Kwahiyo leo wana haki ya kufurahi, kujibaraguza na hata kuogea maji ya bahari kwa kutoa mkosi.

Mwisho niwashauri vijana mnaotaka kuoa changamkieni mabinti ambao ni mashabiki wa Uto. Kama ameweza kuivumilia timu yake kwa miaka 25, hashindwi kukuvumilia wewe na chumba chako kimoja kwa miaka mitano mpaka utakapojenga kwako. Kuanzia kesho kama unatafuta mke "piga sound" binti yeyote aliyevaa kitop cha kijani na shimizi ya njano. Mtanishukuru baadae [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie fanyeni kujifariji ila awamu hii kwa kiwango mlichonacho hata robo katu hamfiki.Ukweli mchungu.
 
Hahahahahahaahahahahaha.....ila kunamashabiki wakolofi sana..sasa huyo wa kwenye picha ndio anajiona aziz kii....!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…