Pengine umeanza leo kufatilia mpira na kuifatilia Yanga, ngoja nikujuze.
Swala la Yanga kushinda ugenini sio kitu kipya kwasababu viongozi, na baadhi ya wachezaji wameshazoea pressure na atmosphere za ugenini.
Yanga imeshinda michezo mingi ugenini mpaka sasa
Kamfunga Tp Mazembe kwake kabisa
Kamfunga Club Africain kwake
Kamfunga Rivers united kwake
Kamfunga Marumo kwake
Kamfunga bingwa wa CAF super cup (USMA) kwake
Hivyo hata Al Merrikh wangekuwa Sudan, isingebadilisha ubora wa kikosi cha Yanga. Yanga anaingia katika haya mashindano akiwa na spirit kubwa sana juu ya kushinda popote pale jambo ambalo linaweza fanya timu zitakazopangiwa nazo kuchukua tahadhari. Club bingwa na shirikisho ni majina tu ya mashindano ila timu zinashahabiana ubora na viwango na ndio maana sio ajabu bingwa wa CAFCL kufungwa na bingwa wa CAFCC.