Yanga dhidi ya Polisi: Nani angefanya nini ili Pius Buswita asifunge goli lile?

Yanga dhidi ya Polisi: Nani angefanya nini ili Pius Buswita asifunge goli lile?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwangu mimi hakukuwa na namna nyingine ya kumzuia mfungaji wa goli lilitosababisha Kaze afukuzwe kazi zaidi ya kusababisha penaliti.

Buswita ni mrefu na alitumia urefu wake kufungu, full stop!!. Matokeo kwenye round ya pili ni hayahaya tu kwa timu zote hasa baada ya timu kufanya makosa ya kuwaacha wachezaji wazuri kilevi kwenye usajili wa dirisha dogo.

Timu zote zimesajili wachezaji wazuri walioachwa kizembe na mabenchi ya ufundi. Wachezaji hawa walioachwa ndio wanaoziangamizi timu zao walizokuwa wakizichezea kwa kucheza kwa nguvu zao zote ili kuzifanya timu zijutie makosa yao ya kuwaacha.
 
Ila ndiyo hivyo sasa. Ameshatimuliwa! Na ni wakati muafaka kwa Viongozi kusajili Mwalimu mwenye sifa na uzoefu wa ligi ya Bongo.

Kiukweli timu yetu ilipoteza mwelekeo tangu walipocheza mechi na Mbeya City kwa kulazimishwa sare kama ya jana. Dakika za majeruhi timu pinzani inasawazisha! Mwalimu hana mbinu za kuihamasisha timu kupata ushindi wa zaidi ya goli moja! Wakipata kagoli kamoja tu, anawaacha wachezaji kurudi kukalinda hako kagoli!

Wakati mwingine, mfano jana anamtoa kiungo mshambuliaji na kumuingiza kiungo mkabaji! Mwisho wa siku timu ikarudi nyuma, na wapinzani kusawazisha. Kimsingi Mwalimu aliishiwa mbinu. Binafsi nimefurahishwa kutimuliwa kwake.
 
Kwangu mimi hakukuwa na namna nyingine ya kumzuia mfungaji wa goli lilitosababisha Kaze afukuzwe kazi zaidi ya kusababisha penaliti.

Buswita ni mrefu na alitumia urefu wake kufungu, full stop!!. Matokeo kwenye round ya pili ni hayahaya tu kwa timu zote hasa baada ya timu kufanya makosa ya kuwaacha wachezaji wazuri kilevi kwenye usajili wa dirisha dogo.

Timu zote zimesajili wachezaji wazuri walioachwa kizembe na mabenchi ya ufundi. Wachezaji hawa walioachwa ndio wanaoziangamizi timu zao walizokuwa wakizichezea kwa kucheza kwa nguvu zao zote ili kuzifanya timu zijutie makosa yao ya kuwaacha.
Afisa Usalama wa Yanga alitakiwa kufanya kitu Ndio maana nae katimuliwa
 
Lakini Senzo si alikuja na faili la Simba sasa inakuwaje tena jahazi laenda mrama?
Nilishasemaga humu jf kuwa kuna timu imetenga fungu kubwa kwaajili ya kupata matokeo mazuri, haijulikani fungu hilo litatumikaje na kwa namna gani, Yanga wasiondoe uwezekano wa jambo hilo, kumfukuza Kaze inawezekana ni sehemu ya hizo pesa maana sioni ni kwa namna gani Kaze anahusika na mchezaji kukosa penaliti au kupoteza nafasi ya kufunga bao wakati amebaki yeye na kipa tu langoni. Katika timu kubwa kama Yanga Kocha kazi yake kubwa ni kuinganisha timu icheze kitimu na kutengeneza nafasi za kufunga magoli lakini sio kumfundisha mchezaji namna ya kuingiza mpira golini. Timu ya Yanga chini ya Kaze inatengeneza nafasi nyingi lakini wachezaji wanashindwa wenyewe kuzigeuza nafasi hizo kuwa magoli.

Tunapomtafuta mchawi wa Yanga kwanza tusiache kuzimulika hilo fungu la pesa za ushindi zimetua kwa nani kwa kupitia nani, pili tuumulike uongozi wa juu wa club na mwisho ndo tuongelee wachezaji.
 
Back
Top Bottom