Yanga haijaishinda Simba katika Ligi ya Bara kwa miaka miwili sasa

Umefanya jambo zuri sana kuweka matokeo ya ligi kuu tu.

Maana ungeweka na yale matokeo ya Ngao ya Jamii kwenye msimu wa mwaka juzi, na msimu huu! Pamoja na yale matokeo ya nusu fainali kombe la shirikisho la Azam msimu uliopita kule Mwanza; naona takwimu zako zingekuwa ni tofauti kabisa.
 
Nimetembea na lugha ile ile mliyokuwa mnatembea nayo utopolo. Mlikuwa mnasema Simba haijaishinda Yanga kwenye mechi za Ligi ya Bara tangu 2019. mlijua kabisa mkisema katika mashindano yote haitanoga, maana tarehe 25/07/2021 Simba iliifunga Yanga 1-0 katika fainali ya Azam Federation Cup kule Kigoma, maana mliona hapa 2021 ni juzi tu. Kwa hiyo na mimi ninazungumzia mechi za Ligi ya Bara, imepita miaka miwili
 
Uko sahihi kabisa! Kwa mara ya mwisho simba mliifunga Yanga 1-0 mwaka 2021 kwenye fainali za ASFC kule Kigoma!

Vipi sasa kuhusu Yanga! Wamewafunga mara ngapi kuanzia hiyo 2021? Naomba uniwekee matokeo yote hapa kama hutojali.
 
Umeleta hoja moja kubwa sana. Upotoshaji kwenye hili suala ulikuwa mkubwa sana. Watu walikuwa wanadanganya mchana kweupe na wengine kutokana na uvivu wa kufuatilia wakabeba uongo huo juu juu.
 
Badala ya Mods kujikita kufungia watu wasiostahili hovyo, wangejikita kupongeza watu wanaoleta nyuzi kama hizi.
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…