kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Yanga inafahamu kuwa kunguru Hana kibiongo, kama ukiona kibiongo basi ameinamatu anaokota kitu.
Wazazi, Ndugu, jamaa, marafiki na wapenda mpira wote lazima wafahamu hili. Yanga ni timu kubwa sana kuweza kumuonea Faisal Salum. Yanga haitapendi kuua kipaji Cha mtoto Fei, LAKINi Yanga inafahamu kuwa Fei Toto haendi kuvua samaki baharini bali anaenda kucheza mpira kwenye timu mojawapo nchini au nje ya nchi baada ya kumalizana na Yanga.
Yanga, wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda mpira wote wanaomtakia mema mtoto Faisal wailani hiyo timu inayomtaka mchezaji nje ya taratibu za mpira.
Kama hiyo timu haramu itafanikiwa kumpata mchezaji kwa njia hii baasi mpira wetu utavurugika sana. Kila timu itatumia njia hii kupata wachezaji inayowataka.
Chaajabu hakuna anaeitaja Wala kuitafuta hii timu inayomtaka Faisal kwa njia hii, sio Wazazi wake Faisal, ndugu, mawakili wala TFF. Wala hakuna mtu anaetaka kujua Yanga imepata hasara gani kwa kumlea na kumkosa mchezaji wake kwa muda huu wote. Wala hakuna anaetaka kujua ni wapi Fei Toto alipata pesa za kununulia mkataba wake kwa njia haramu kabisa.
Yanga wako Smart, hiyo timu haramu ilidhani watampata Fei Toto kwa mchezaji kufukuzwa Yanga, au kupewa adhabu ya kulipa fidia. Kifupi Fei Toto, hiyo timu, mawakili, wazazi, wapambe na hata TFF wamenasa kwenye urimbo wa Yanga hadi 2024.
TFF kuruhusu Fei Toto kuitwa timu ya taifa maana yake na wao ni kati ya wadau ambao wamenasa kwenye mtego wa Yanga, wanasononeka sana Fei na "timu yake" mpya kunasa kweñye mtego wa Yanga, na wakati huohuo Yanga inaelekea kutwaa ubingwa bila Fei Toto.