kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #21
Kaka haya ni maajabu makubwa kuwahi kutokea, waliomfukuzuza hawakuangalia maslahi mapana ya Yanga, walitanguliza ubinafsi na umimi. Kijana Zahera alitupa raha wanayanga katika kipindi kigumu sana hata tukashinda nafasi ya pili nyuma ya matajiri Simba na mbele ya matajiri Azam. Alihaha huku na kule kuibakiza furaha ya wanajangwani, nadhani ni mapema mmo kumfukuza Zahera, kipaumbele kingekuwa kutafuta pesa za kumlipa Dante arudi kuichezea club, kuwatibu majeruhi warejee uwanjani, kutafuta vibali vya wachezaji wa kigeni na kutafuta vyanzo vya uhakika ili kujenga uwanja wa mazoezi.Yaani mnafukuza mfadhili? Mtapata tabu sana.