Mi nasema,kama kweli serikali ndiyo iliwaomba TFF wasogeze mechi,basi kitendo cha yanga kutoitambua mechi ya tarehe 3 ni kitendo cha uasi dhidi ya serikali.
Kama serikali haikutoa maelekezo,basi ni wakati muafaka kutoka hadharani na kukemea vikali tabia ya taasisi nyeti kama TFF kuisingizia katika jambo kama hili kwa maslahi ya timu moja.
Hadi sasa sijaona kama serikali imekanusha kusingiziwa kwenye hili.
Kama walishauri bila kujua kanuni zinasemaje,na hawakuwa na sababu ya msingi,walipaswa kuiamuru TFF ikanushe barua yake ya kuahirishwa kwa mechi huku serikali ikisingiziwa.Vinginevyo kama walisingiziwa na wakanyamaza,Katibu mkuu wizara ya habari na michezo anapaswa ajiuzuru kwa kushindwa kuingilia kati suala la serikali kuchafuliwa kwa kusingiziwa na TFF kwa jambo ambalo haikulifanya.Ulikuwepo muda wa kulifanyia kazi kabla ya saa 11.
Ila kama kweli serikali inajua ilihusika,basi viongozi washabiki wa yanga waliopo serikalini,waishauri timu yao isijipime nguvu na serikali.Kama wanaruhusu hivyo,basi hawana nia njema na Rais wetu.Nitaanza kuwa na mashaka nao