Yanga hawatafurukuta CAFCL.

Yanga hawatafurukuta CAFCL.

Vawulence

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
1,930
Reaction score
2,118
Baada ya kuangalia mchezo wa leo baina ya Simba na Yanga, ni dhahiri yanga hawana timu ya kufanya maajabu ligi ya mabingwa msimu ujao.
Timu imejengwa kumzunguka mtu mmoja tu kiasi kwamba akishadhibitiwa basi tu inatepeta.
Simba ndio kipimo cha watakachokutana nacho ligi ya mabingwa. Kama Yanga wako serious wanatakiwa kusajili hasa wachezaji wenye uwezo wa kuamua michezo migumu. Sio hawa kina sure boy..

roho mbaya.PNG
 
View attachment 2206582
Kwa mtiririko wako wa hoja iko hivi, Yanga hawezi kufurukuta Club bingwa kwa sababu kashindwa kumfunga Simba. Simba ambaye naye kashindwa kumfunga Yanga alifika robo fainali.
Kwa mantiki hiyo, Simba na Yanga viwango vyao kwa sasa ni vya kuishia robo fainali.
 
Baada ya kuangalia mchezo wa leo baina ya Simba na Yanga, ni dhahiri yanga hawana timu ya kufanya maajabu ligi ya mabingwa msimu ujao.
Timu imejengwa kumzunguka mtu mmoja tu kiasi kwamba akishadhibitiwa basi tu inatepeta.
Simba ndio kipimo cha watakachokutana nacho ligi ya mabingwa. Kama Yanga wako serious wanatakiwa kusajili hasa wachezaji wenye uwezo wa kuamua michezo migumu. Sio hawa kina sure boy..

View attachment 2206582
Mlianza na kusema round ya pili mnaamka, haya round ya pili ndio hiyo ina yoyoma, mara hoo mkasema mechi nne yanga atapoteza ikiwemo ya Azam zote Yanga kashinda, mara hoo mkasema mtiapiga ya Yanga kwa mkapa mechi droo. Leo naona mmehamisha magoli kwenye CAF champions, kwani nyie kwa usajili alio ufanya Yanga msimu mliopita mmlishawahi kufikiria msimu huu Yanga itakuwa hivi, tena na muunganiko mkubwa wachezaji wamelewana ndani ya mda mfupi na kuipa matokeo Yanga.

Pambaneni na timu yenu na viongozi wenu ambao wamechemka kwenye kusajili (sijui wamekula 10%),Mwenyekiti wenu anahojiwa na EFM anadai "Simba ya msimu huu ni bora zaidi ya msimu uliopita ".Msimu huu mmekosa ubingwa, mmedrop kutoka Klabu bingwa mpaka shirikisho. Mkae mjipange wachezaji kibao (zaidi ya 10) mikataba yao ishaisha mmoja wapo Manula kwa saves alizozifanya lazima atataka fungu kubwa,mambo ya kiwaga magumu mnakumbushiaga bil 20.

Mnakazi ya kuoffload timu yenu, kufanya usajili mpya (hapo ndipo viongozi wenu wanapompigaga MO) na baada hapo mtengeneze muunganiko kwenye timu.

Yanga ndio tushachukua ngao, sasa hivi ligi bado Azam Confederation dadadedekiiiiiii......
 
Back
Top Bottom