Yanga ibadili rangi ya jezi

Yanga ibadili rangi ya jezi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwakuwa Yanga ni club yenye wanachama na mashabiki mbalimbali bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa Je, Kuna madhara gani kama club ya Yanga ikibadili rangi ya jezi yake ili isifanane na rangi za jezi za vyama vya siasa nchini?
 
Ibadili rangi iliokiwanayo toka mwaka 1935 kwa sbb ya hao waliowaiga mwaka 1977? Hiyo akili matope
 
Ibadili rangi iliokiwanayo toka mwaka 1935 kwa sbb ya hao waliowaiga mwaka 1977? Hiyo akili matope

Hiyo siyo hoja, zipo club kubwa na kongwe kama Barcelona ambazo zimewahi kubadili rangi zao za jezi kwa sababu zao za msingi. Yanga pia ina sababu ya msingi ya kuibadili rangi ya jezi yake kwa kuwa Hii rangi ya jezi ya Yanga huwa ina mislead wadau, kwani rangi hii inafanana kabisa na rangi ya chama cha siasa cha CCM, kuna wakati hata yale matawi ya Yanga mitaani unaweza kudhani kuwa ni matawi ya wakereketwa. Kwanini Club pia isiende na wakati kutokana na mabadiliko yanayotokea nchini na duniani? Kuna wanachama na mashabiki wanaoshindwa kununua na kuvaa jezi za Yanga kwasababu ya rangi yake.
 
Kusema kweli mm ni shabiki wa Yanga ila kwenye suala hili la jezi; huwa nafumba macho tu na kujisahaulisha. Sizipendi kinoma
 
CCM ni laana..Ukivaa kitu chenye rangi za CCm lazima upatwe na laana..

Yanga wanalaana..
 
CCM ni laana..Ukivaa kitu chenye rangi za CCm lazima upatwe na laana..

Yanga wanalaana..
Na unakua na fikra za hivi kila wakati...
10982295_1030857820274946_8680615381328160391_n.jpg
 
Kusema kweli mm ni shabiki wa Yanga ila kwenye suala hili la jezi; huwa nafumba macho tu na kujisahaulisha. Sizipendi kinoma
Mko wengi kwenye hilo, jezi, kofia, skafu, tracksuit na bendera za yanga vyote vinawakorofisha baadhi ya wadau. Kama club ya Yanga inadhamilia kuongeza mapato ya club kwa kuuza jezi na vifaa vya Yanga haina budi kulifikiria suala hili kabla haijakuwa na ndoto hiyo. Mbeya City ni timu mpya lakini jezi zake zimekubalika haraka kutokana na rangi
 
Rangi ya kijani ni rangi ya majani na matunda (amani) ambayo yanapendwa kuliwa na viumbe wengine wote. Kinyota rangi ya njano/kijani ni rangi ya nyota ya kondoo/mbuzi wanaoweza kutafunwa na simba, chui, fisi n.k. bila upinzani mkubwa.
 
Back
Top Bottom