Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

Kuruka juu ya viti haijawahi kuwa kosa la kisheria au kiusalama katika mpira sehemu yoyote duniani ila kurusha chupa, kiti au kitu kingine chochote kwa nia ya kumdhuru mshabiki mwenzio, mara nyingi tu adhabu zimetolewa kwa makosa hayo. Najua hilo unajua. Sitegemei kama unawabishia hivyo walimu wako huko shuleni, labda kama unawapa tabu kwa mambo mengine.
Kweli wahenga walisema akili ni nywele ila hawa kuidentify za eneo lipi.
 
Kama picha za video zipo, YANGAwazikabidhi polisi, watafutwe hao wahuni. No matter ni mashabiki wao au wa jirani.
Wakishakutiwa nguvuni walipishwe.
YANGA mnakubali vipi kuharibiwa jina.
 
Haya sasa, taarifa imeshatoka kwa Yanga kutakiwa kulipiga gharama za uharibifu. Sijui wale wafia timu mna lipi la kusema.
joseph1989 Southern Highland na wengine....

Yanga yatakiwa kugharamia viti vilivyongo'olewa
Source: Clouds TV

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imewasilisha malalamiko rasmi kwa TFF na kuwataka Yanga kugharamia uharibifu uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wao dhidi ya Al Ahly .

Barua ya Wizara inasema:

Wizara ilitoa kibali cha kufanyika kwa mchezo wa kimataifa kati ya Yanga SC (Tanzania) dhidi ya Al-Ahly (Misri) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliofanyika tarehe 2 Desemba, 2023 majira ya Jioni.

Hata hivyo, Wizara imepokea Malalamiko kutoka kwa Uongozi wa Uwanja ambapo mashabiki wa Klabu ya Yanga wanalalamikiwa kwa kuwasha fataki wakati mchezo ukiendelea na kusababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya viti kung’olewa.

Wizara inakemea vikali kitendo hiki na kuwataka Klabu ya Yanga mara moja kuwasiliana na Uongozi wa Uwanja ili kuweza kubaini ukubwa wa tatizo na kuona namna bora ya kulitatua.

Kwa barua hii, Wizara inawasilisha rasmi malalamiko haya kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa ndiye mdhamini wa vilabu hivi kwa maombi ya matumizi ya Uwanja huu ili kuwajulisha Klabu ya Yanga SC kuwa inapaswa kugharamia matengenezo ya viti vilivyong’olewa na Mashabiki wakati wa mchezo huu.

Aidha kuwaonya mashabiki wao kuacha mara moja tabia hizi ili uendelea kustawisha michezo
na kuulinda Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Wafanya fujo tunawajua ni kina nani siku zote. Hawajifichi wala kuona haya kuonyesha umbumbumbu wao kwa hili nakiri makolo ilikua mbinu ya kutukomoa ili mradi kupunguza machungu ya zile tano zilizoambatana na mabango ambayo yalizidi kuongeza uchungu. Hongereni sana pamoja viongozi wenu wafanya maamuzi walioamua haya
 
Wafanya fujo tunawajua ni kina nani siku zote. Hawajifichi wala kuona haya kuonyesha umbumbumbu wao kwa hili nakiri makolo ilikua mbinu ya kutukomoa ili mradi kupunguza machungu ya zile tano zilizoambatana na mabango ambayo yalizidi kuongeza uchungu. Hongereni sana pamoja viongozi wenu wafanya maamuzi walioamua haya
Hakika ujinga wa uzeeni lazima utakufa nao tu pole sana
 
Back
Top Bottom