Yanga ikiiondoa Al Hilal, nchi haitakalika Jumamosi

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kusema kweli kwa namna Yanga inavyobezwa na kuonekana kuwa tayari imeshaondolewa kutokana na rekodi za Wasudan hao wanapokuwa kwao, wakati ina wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo muda wowote. Sipati picha siku hiyo ya Jumamosi jioni inafika dakika ya 90 bila bila.

Refa anaongeza dakika 3 tu, Al Hilal wanafanya shambulio la hatari, Bangala anaokoa anaitupia kwa Morrison, Morrison anamlamba mtu chenga anairusha kwa Kisinda, dakika ya 92 na sekunde, Kisinda anairusha kwa Fiston Mayele, mwamba haitulizi, anainyoosha moja kwa moja had kimiani, Yanga 1 Al Hilal 0.

Siku hiyo kutakuwa na maandamano nchi nzima, nchi haitakalika.Tuombe mungu jamani.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Hebu tuangalie ubora wa timu wanazopangiwa Simba hatua za awali na wanazopangiwa Yanga sijawahi kuona Simba wakipewa TP Mazembe, Asante Kotoko, Asec Mimosas, Al Ahly, Kaizer Chiefs au Raja Casablanca hapa kuna mchezo wa kuipaisha Simba kimataifa!!

Kitu kizuri wanapotoboa makundi wanakutana na timu jiwe safari yao na tambo zinaisha!!
 
Ipo siku ukweli utajulikana.
 
Mpira sio illusion naona unafumba macho unafikiria iwe hivyo. Mnavyotaman kufuzu ugenini wasudan nao wanatamani kufuzu nyumbani. Wenzenu wakicheza mechi za kirafikie za kimataifa na Simba na Asante Kotoko na TP Mazembe kote huko mlikuwa mnawachambua kwa macho tu huku nyie mkicheza na Mbuni FC as if mnajiandaa na FA ya Azam Cup
 
Zolan ndo team kubwa
 
Yanga lialia
 
We mwenyewe umakiri kuwa hupati picha ya hicho unachojaribu kuwaza, bab yenu Manara amewaambia muende kule sudan kama underdogs na sio magiants.

Nadhani akili imewakaa vizuri sasa.
 
Co rahc hvyo bwashee
 
Tatizo la uto ni ule mwiko uliopo nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…