Yanga ilikosa Ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988 ili tu amsaidie Simba isishuke daraja!

Yanga ilikosa Ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988 ili tu amsaidie Simba isishuke daraja!

Simba Ilinusurika kushuka 1987,1988,1989 kama uamini muulize Baba Yako au Babu Yako kama alikua mpenzi wa soka.
 
Ushindi wa goli 2 - 1 wa Simba dhidi ya Yanga Julai 23, 1988 katika Uwanja wa Uhuru, ndio uliowanusuru Simba kushuka daraja na kumaliza na pointi 20, mbili zaidi ya Tukuyu Stars.
Ili kufupisha stori, Yanga ilifungwa 2-1 na Simba
 
Hicho kitu nimesikia hadi makongoro nyerere anaongea, sijui kina ukweli kiasi gani!
 
😂😂😂
Dar es Salaam, 1988

▶️Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba akimkabidhi tuzo ya Mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu mwaka 1988, kiungo wa Yanga, Athumani Abdallah China.View attachment 3166496

▶️Katika msimu huo, Coastal Union ya Tanga iliibuka bingwa baada ya kuizidi tu wastani wa mabao Yanga, huku Simba ikinusurika kushuka daraja baada ya kumaliza juu ya Tukuyu Stars ya Mbeya na Reli ya Morogoro zilizoteremka daraja.

▶️Ushindi wa goli 2 - 1 wa Simba dhidi ya Yanga Julai 23, 1988 katika Uwanja wa Uhuru, ndio uliowanusuru Simba kushuka daraja na kumaliza na pointi 20, mbili zaidi ya Tukuyu Stars. Mabo ya Simba yalifungwa na Edward Chumila dk ya 21 na John Makelele dk 58, huku goli la Yanga lilifungwa na Issa Athumani dk 36.

Za ndaaani zinasema Yanga ilimsaidia mtani asishuke daraja.
😂Kumbe vipigo viliwaanza muda sanaa.
Hata tungeshuka tungepanda tena.
Nyie semeni mlinyukwa 2 - 1 wakati mkitarajia kuchukua kombe
 
Labda ulisimuliwa, wengine tulikuwa uwanjani, Simba ilihitaji kushinda isishuke daraja na yanga ilihitaji ushindi ichukue ubingwa.
Kama walimwachia Simba kwanini Sahau Kambi walimwacha msimu unaofuata.
Mkifungwa huwa hamkosi sababu.
Tuliokuwepo bado tupo, tafuta wa kuwadanganya,Simba hata wangefungwa na Yanga wasingeshuka daraja maana wangebaki na points 18 na magoli ya kufunga 25 (ambayo ndio ilikuwa kigezo cha pili baada ya kulingana points na sio GD ya sasa hivi).Timu zilizoshuka ni Tukuyu Star na Railways,Tukuyu ambayo ndio mshindani wa karibu wa Simba asingeweza kumshinda Simba maana alikuwa na magoli 16,Hata kama kigezo cha GD kingetumika,Simba walikuwa na GD ya 0 na Tukuyu Star -3 . Kumbuka timu iliyoshinda ilikuwa inapata points 2 na sio 3 za sasa. Pili, kama lengo la Yanga ni kuinusuru Simba wasingehangaika kutafuta bao la kusawazisha la Issa Athumani, wangecheza bila kushambulia, tatu, goli linalolalamikiwa ni goli la pili la John Makelele ambalo mnamlaumu Sahau Kambi,hivyo kama si goli hilo matokeo yangebaki 1-1 na hivyo Simba kuwa na points 19,juu ya Tukuyu na Reli, maana goli la kwanza la Edward Chumila halilalamikiwi popote.
 
Attachments

  • Screenshot_20241203-073008.png
    Screenshot_20241203-073008.png
    669.6 KB · Views: 6
Kaduguda mwenyewe amekiri hili kuwa Yanga waliwaachia ili Simba isishuke daraja
 
Wewe na KADUGUDA nani anaijua Simba?
Angalia msimamo huu halafu useme ni vipi Simba angeshuka daraja kwa kufungwa na Yanga, ukizingatia kwa wakati huo timu iliyoshinda ilikuwa inapata points 2.Kwa hiyo Simba angefungwa na Yanga wangebaki na points 18 na magoli ya kufunga 25.Kigezo cha kwanza timu zikilingana points kilikuwa magoli ya kufunga,Simba ilikuwa na 25 na Tukuyu 16,ni timu mbili ndio zilitakiwa kushuka daraja.Tumia akili yako na si ya Kaduguda
 
Attachments

  • Screenshot_20241203-073008.png
    Screenshot_20241203-073008.png
    669.6 KB · Views: 3
Angalia msimamo huu halafu useme ni vipi Simba angeshuka daraja kwa kufungwa na Yanga, ukizingatia kwa wakati huo timu iliyoshinda ilikuwa inapata points 2.Kwa hiyo Simba angefungwa na Yanga wangebaki na points 18 na magoli ya kufunga 25.Kigezo cha kwanza timu zikilingana points kilikuwa magoli ya kufunga,Simba ilikuwa na 25 na Tukuyu 16,ni timu mbili ndio zilitakiwa kushuka daraja.Tumia akili yako na si ya Kaduguda
Tukuyu alifungwa mechi ya mwisho akabaki na point zake 18 ila angeshinda Angekuwa na point 20 na Simba angefungwa angebaki na 18 mbona ni jambo lililo kua wazi kwa kipindi kile kwamba kama Yanga ita komaaa Simba ata shuka.

Kumbuka baada ya kufungwa na Pamba mechi Moja kabla ya hii ya mwisho kule Mwanza, Viongozi walikimbia timu, alibaki Shika mkono pekeyake, Mwenyekiti Bwana Jimmy David Ngonya Alisha sepa na wajumbe wake.
Lilikua jambo la ku ogofya na kutia Simanzi ukumbuke Yanga ilikua ya moto Sana.
Simba ilikua inafanya vibaya na migogoro isiyo isha.
Hii ni Moja ya sababu ilipelekea Tajiri mzee Shika Mkono kufirisika.
Yeye ndiye Ali ihudumia timu na Ali iweka kambini kule Hoteli ya Njuweni Kibaha kabla ya Mechi.
Ilifikia Mzee kuzimia wakati anaileta timu pale Taifa siku ya Mechi iyo na Yanga, ilibidi Gari la wachezaji liendeshwe na wachezaji, Chumila/Makelele unaweza pata picha Hali ilikua ya kuti sha kwa kiasi Gani.

Ili leta shida kwa uongozi wa Yanga mpaka Serikali ili ingilia kati.
Ata baadhi ya wachezaji waligawanyika kwakua uongozi wa Yanga ulikua ume gawanyika kuhusu swala ilo.

Ukumbuke Simba wakati wanajitoa ndani ya Yanga mwaka 1936 ili leta tabu Sana baina ya mashabiki ila mkoloni alifanikiwa.
Ili leta mpasuko mkubwa kwakua ivi vilabu mikusanyiko yake kwa vijana na wazawa vilihusika kukusanya watu na kupenyeza Ajenda za kutafuta uhuru.
Mpaka ilipofika miaka ya mwishoni mwa 50 Nyerere na wenzake walipo kuja na kuamua kupunguza mpasuko kwa Kundi ilo la vijana na baadhi ya Wazee wa ki bantu kwa kuamua wao kama viongozi wakubwa wa Tanu wagawanyike.

Wengine wakina Kawawa na wenzake wajiunge na upande wa Simba ili wapate taarifa za uhakika upande uo wa mkoloni unafanya Nini katika harakati izo za uhuru.

Tukumbuke Wakati uo Mwingereza ndio alikua mtawala na sera yake ilikua Divide and rule kwaiyo waliamua kuigawanya Yanga baada ya kuona tishio katika harakati za uhuru na kufanikiwa kui pasua kiasi kwa kupata baadhi ya wazawa kuanzisha timu Yao mpya ya Queens japo wahindi ndio walikua wafadhili wa Queens ambayo ki uhalisia ni maagizo ya Gavanor(Mtawala) wa Uingereza.

Jina ilo lilikua la kuji komba kwa Malkia mtawala wa Uingereza lililo tolewa na Viongozi machwa (Wahindi) waliokua Wana Nyazfa kwenye Serikali ya Mzungu.
 
Tukuyu alifungwa mechi ya mwisho akabaki na point zake 18 ila angeshinda Angekuwa na point 20 na Simba angefungwa angebaki na 18 mbona ni jambo lililo kua wazi kwa kipindi kile kwamba kama Yanga ita komaaa Simba ana shuka.

Ili leta shida kwa uongozi wa Yanga mpaka Serikali ili ingilia kati.
Ata baadhi ya wachezaji waligawanyika kwakua uongozi wa Yanga ulikua ume gawanyika kuhusu swala ilo.

Ukumbuke Simba wakati wanajitoa ndani ya Yanga mwaka 1936 ili leta tabu Sana baina ya mashabiki ila mkoloni alifanikiwa.
Ili leta mpasuko mkubwa kwakua ivi vilabu mikusanyiko yake kwa vijana na wazawa vilihusika kukusanya watu na kupenyeza Ajenda za kutafuta uhuru.
Mpaka ilipofika miaka ya mwishoni mwa 50 Nyerere na wenzake walipo kuja na kuamua kupunguza mpasuko kwa Kundi ilo la vijana na baadhi ya Wazee wa ki bantu kwa kuamua wao kama viongozi wakubwa wa Tanu wagawanyike.

Wengine wakina Kawawa na wenzake wajiunge na upande wa Simba ili wapate taarifa za uhakika upande uo wa mkoloni unafanya Nini katika harakati izo za uhuru.

Tukumbuke Wakati uo Mwingereza ndio alikua mtawala na sera yake ilikua Divide and rule kwaiyo waliamua kuigawanya Yanga baada ya kuona tishio katika harakati za uhuru na kufanikiwa kui pasua kiasi kwa kupata baadhi ya wazawa kuanzisha timu Yao mpya ya Queens japo wahindi ndio walikua wafadhili wa Queens ambayo ki uhalisia ni maagizo ya Gavanor(Mtawala) wa Uingereza.

Jina ilo lilikua la kuji komba kwa Malkia mtawala wa Uingereza lililo tolewa na Viongozi machwa (Wahindi) waliokua Wana Nyazfa kwenye Serikali ya Mzungu.
Unaongea nadharia, kwamba ili Simba ashuke daraja ilitegemea factors nyingi, kwamba ilibidi nao Tukuyu Star wafungwe na zaidi walikubali kushuka daraja ili Simba wabaki,unawachukuliaje Wanyambala?nategemea utaleta bla blah nyingine pia kuwa Tukuyu Star nao walikubali kufungwa ili kuibeba Simba,mie pia nilikuwepo, hiyo habari ilisemwa lakini haikuwa na uhalisia. Yanga waliineza zaidi kwa sababu waliumia kukosa ubingwa kwa kuwa na mogoli machache ya kufunga. Miaka ya karibuni hapa pia Simba walichukua ubingwa kwa Yanga na Mtibwa waliokuwa wa kwanza na wapili, Simba aliyekuwa wa tatu alichukua ubingwa bila kutarajia. Hayo mambo huwa yanatokea. Sasa nyie mnadanganya watoto kwa kuwaaminisha vitu vya kufikirika tu. Sasa kama walitaka kuinusuru Simba kwa nini walikuwa wanashambulia na kusawazisha goli? Kwa nini walimfukuza Sahau Kambi kama mwenzako anavyodai maana amefanya kazi yake aliyoagizwa ya "kuinusuru" Simba
 
Kwanza sahau Kambi hamufukuzwa ila aliachwa kwa msimu unao fuatia, kwakua ulikuwepo uwanjani basi nikumbushe Magoli ya Simba yalifungwa kaskazini au kusisini mwa uwanja ili usini choshe tafadhali na mlinda mlango wa Simba na mabeki wake wa 4 walio mzunguka.
 
Back
Top Bottom