SI KWELI Yanga imetangaza kuachana na kocha wake Saed na kocha wa viungo Mustafa

SI KWELI Yanga imetangaza kuachana na kocha wake Saed na kocha wa viungo Mustafa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kimeumana jangwani
1000214156.jpg
 
Tunachokijua
Young Africans Sports Club (Yanga) ni timu ya mchezo wa mpira wa miguu inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara ambayo ilianzishwa mwaka 1935. Tangu kuanzishwa kwake timu hiyo imetwaa ubingwa wa ligi hiyo mara thelathini (30) mafanikio ya timu hiyo yamechangiwa na watu mbalimbali ikiwemo walimu (makocha) ambao wamekuwapo kwa nyakati tofauti.

Ni kawaida kwa timu za mpira wa miguu kubadilisha makocha mara kwa mara ili kuimarisha ubora na kujenga vikosi vyenye uwezo wa kushindana katika mashindano na ligi mbalimbali.

Timu ya Yanga Baada ya kuwa na mwenendo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha, mnamo tarehe 15, Novemba 2024 uongozi wa Yanga ulivunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Angel Miguel Gamondi pamoja na kusitisha mkataba wa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw. Masaa machache baadaye Yanga walimtangaza Kocha Mkuu mpya Sead Ramovic akichukua mikoba ya Gamondi.

Kumekuwapo na taarifa hivi karibuni kuwa Yanga wametangaza kuvunja mkataba wa kocha huyo mpya Sead Ramovic pamoja na kocha wake wa viungo Mustafa Kodro.


Je uhalisia wa taarifa hiyo ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii wala kutolewa sehemu nyingine yoyote na Klabu ya Yanga.

Hata hivyo chapisho hilo la taarifa kwa umma limebainika kuwa lilihaririwa kutoka kwenye taarifa rasmi ya Yanga iliyotolewa kuhusu kuvunjwa kwa mkataba wa kocha mkuu, Miguel Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw.

Pamoja na hayo yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanalitofautisha chapisho hilo dhidi ya taarifa rasmi ambazo hutolewa na Yanga, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na matumizi ya mwandiko (fonts) usiotumiwa na timu hiyo katika taarifa zake rasmi kwa umma.

Hata hivyo tarehe 12 Disemba Kocha mkuu wa timu hiyo Sead Ramovic alionekana akiongoza mazoezi ya timu hiyo ikifanya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Hivyo taarifa hiyo ya kuvunjwa kwa mikataba kwa makocha hao si ya kweli.
mbona hii taarifa haipo kokote hata kwenye page rasmi za Yanga?
 
Back
Top Bottom