Yanga ina kikosi imara sana

Yanga ina kikosi imara sana

B I N A M U

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
1,495
Reaction score
2,403
Kikosi cha yanga kwa Muda waliokaa kambini ni Mchache sana na ukizingatia Safari za hapa na pale!

1st Goalkeeper, Djigui Diarra ni bonge Moja la Mchezaji, hata uwe mnafiki vipi Lazima kazi yake utaikubali tu, Magoli aliyofungwa ni Makosa ya kimpira tu Tumpe Mechi Tano tu Then ndio tuanze Lawama za Kibongo!

2nd, Natamani Combination ya Dickson Job na Bakari Nondo iendelee kuaminiwa Maana ni Hazina ya Taifa, Naamini kwa Siku za usoni itakua Bora kabisa

3rd Natamani Nione Combination ya Double Pivot ya Mukoko Tonombe na Yannick Bangala, Hii itakua ni Safu Bora katika kuimarisha Ulinzi kwa kuwasaidia Job na Nondo!

4th: Djuma Shabani ni Namba Nyingine kabisa, Shomari Kibwana ameletewa Mwalimu sahihi wa Kumpa Changamoto ni wakati sahihi wa kutambua Majukumu yake!

5th: Kocha Jana alifanya makosa makubwa sana, Jana tulitamani sana tuone kushoto tuna Nini, Tuna Mchezaji mpya kule kwenye beki ya Kushoto tulitaka tumuone nayeye anakipi kwa wananchi! Japo Shomari Alifiti lakini tulitaka tuone mtu wa Nafasi ile.

6th: Feisal Abdallah Salum "Toto" kwa Kifupi unaweza Muita " F A S T" Sina Maneno Mengi zaidi ya kusema "He is professional Maestro" Kocha kajua kumtumia.

7th: Left Wing, Farid hatoshi kabisa, Faridi ni yuleyule wa Mwaka jana, Anahitaji Mwalimu bora wa Saikolojia.

8th: Jesus Moloko, Kuna watu wanajaribu kumponda huyu Bwana mdogo, Mimi nasema Hapana, Tumpe muda Angalau Mechi hata Kumi, Kwangu Mimi he is SUPER PLAYER! Ukitaka kujua hilo angalia mikimbio yake yuko vizuri!

9th: Makambo ni yuleyule Makambovic🔥🔥, Na safari hii anawatu kweli kweli! Kwahiyo Tusubiri tu Furaha Msimu huu!

10th: Fiston Mayele Sina wasiwasi naye ni pressure tu jana ilimgharimu ila pia Wananchi Muwe na Subira juu yake! Wanaomponda ni wale wa upande wa Kikeni kikubwa ni Support tu!

=> Zawadi Mauya Nafasi yako iko mashakani Maana kuna watu wa kazi
  • Mukoko Tonombe
  • Yannick Bangala
  • Khalid Auco
ASANTE SANA GSM
 
Yanga ilijiandaa kwa ajili ya Tamasha la utambulisho wa wachezaji na Haji Manara tu.

Haikuiandaa timu kwa ajili ya ushindani wa michezo ya CAF. Bado haina ubavu wa kufanya vizuri. Wachezaji wote ni wazuri ila bado wataishia kucheza vizuri dakika 45 tu. Mpaka mje mkae sawa mtakuwa mshachelewa.
 
Wachezaji ni wazuri, changamoto timu haijaandaliwa, lazima yanga mkubali kupitia kipindi kigumu haswa game za mwanzo mwanzo.. Muombe mungu awe upande wenu dhidi ya wanaijeria katika caf mkipenyaa hapo naimani round inayofuata mtakuwa mmeunga, ligi itakuwa ishaanza..
 
Ayo unasema wewe
Yanga ilijiandaa kwa ajili ya Tamasha la utambulisho wa wachezaji na Haji Manara tu.

Haikuiandaa timu kwa ajili ya ushindani wa michezo ya CAF. Bado haina ubavu wa kufanya vizuri. Wachezaji wote wazuri ila bado wataishia kucheza vizuri dakika 45 tu. Mpaka mje mkae sawa mtakuwa mshachelewa.
 
Time will tell
Wachezaji ni wazuri, changamoto timu haijaandaliwa, lazima yanga mkubali kupitia kipindi kigumu haswa game za mwanzo mwanzo.. Muombe mungu awe upande wenu dhidi ya wanaijeria katika caf mkipenyaa hapo naimani round inayofuata mtakuwa mmeunga, ligi itakuwa ishaanza..
 
Kwaiyo hao viongozi hawakuona umuhim wakuweka kambi mapema ? Yani nyie utopolo kila siku nikujitetea sijui lini mtakua serious
 
Miaka mi 3 Sasa GSM anatufanya yanga ma bwenge ntozeni wake.kila mwaka usajili wa wachezaji zaidi ya 9 kila mwaka tuipe muda timu,brooh ujinga una mwisho wake.
 
Yanga imesajili vizuri lakini tatizo ni uongozi na GSM. Hawajui wafanye nini kwa wakati gani. Mpaka sasa hivi Yanga ilitakiwa iwe imeshafanya mazoezi ya kutosha ya pamoja na kupata walau mechi tatu za kimataifa ili kujenga muunganiko na kurekebisha mapungufu. Lakini wapi matokeo yake wameenda kuzurura Moroco wamerudi hapa wamecheza mechi mbili na timu za madaraja ya chini badala hata kutafuta mechi na timu za ligi kuu. Na sasa hivi wachezaji wapo kwenye timu zao za taifa wakirudi Yanga itakuwa na kama wiki moja tu ya kufanya mazoezi ya pamoja kabla haijakutana na Rivers ya Nigeria kitu ambacho ni hatari sana kwao.

Kama viongozi wa Yanga wangekuwa imara naamini kabisa wangemshauri vizuri GSM kuhusu mambo ya kiufundi kama kambi na mechi za kirafiki badala ya kumuacha atumie muda mwingi kwenye kuuza jezi. GSM ajulishwe tu kuwa jezi atauza mpaka achoke iwapo atawekeza kwa nguvu zote kwenye timu iwe inacheza mpira wa kuvutia na inapata matokeo mazuri na kukusanya makombe na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom