Yanga ina kikosi imara sana

Yanga ina kikosi imara sana

Yanga imesajili vizuri lakini tatizo ni uongozi na GSM. Hawajui wafanye nini kwa wakati gani. Mpaka sasa hivi Yanga ilitakiwa iwe imeshafanya mazoezi ya kutosha ya pamoja na kupata walau mechi tatu za kimataifa ili kujenga muunganiko na kurekebisha mapungufu. Lakini wapi matokeo yake wameenda kuzurura Moroco wamerudi hapa wamecheza mechi mbili na timu za madaraja ya chini badala hata kutafuta mechi na timu za ligi kuu. Na sasa hivi wachezaji wapo kwenye timu zao za taifa wakirudi Yanga itakuwa na kama wiki moja tu ya kufanya mazoezi ya pamoja kabla haijakutana na Rivers ya Nigeria kitu ambacho ni hatari sana kwao.

Kama viongozi wa Yanga wangekuwa imara naamini kabisa wangemshauri vizuri GSM kuhusu mambo ya kiufundi kama kambi na mechi za kirafiki badala ya kumuacha atumie muda mwingi kwenye kuuza jezi. GSM ajulishwe tu kuwa jezi atauza mpaka achoke iwapo atawekeza kwa nguvu zote kwenye timu iwe inacheza mpira wa kuvutia na inapata matokeo mazuri na kukusanya makombe na si vinginevyo.
Simba amecheza mechi na timu gani kubwa za kimataifa ebu tutajie hapa? Manake Simba nae ameuza baadhi ya wachezaji na amesajili wengi tumemsikia kocha wa Simba nae akisema anahitaji muda kutafuta muunganiko wa kikosi chake kwani Kuna mabadiliko mengi.Yani kwa sababu Yanga kufungwa kwenye Bonanza ndiyo kelele zote hizo,hivi akimfunga Rivers utd mtaweka wapi sura yenu wachambuzi kama wewe? Acheni maneno maneno kumbuka Nabi ni kocha mzuri anajua anachokifanya nyie subiri dozi kwenye msimu huu.
 
Sema tu mwalimu anazingua kuwaacha mabeki namba 3 halisi kama yule mgeni Bryson, Adeyun na Mustafa! Na kumchezesha Kibwana Shomari!

Mechi zijazo Zawadi Mauya na Faridi Musa ni vyema wakaanzia nje. Tunahitaji maingizo mapya.
 
Adeyun daaah sioni mchezaji ndani yake
Sema tu mwalimu anazingua kuwaacha mabeki namba 3 halisi kama yule mgeni Bryson, Adeyun na Mustafa! Na kumchezesha Kibwana Shomari!

Mechi zijazo Zawadi Mauya na Faridi Musa ni vyema wakaanzia nje. Tunahitaji maingizo mapya.
 
𝗗𝗔𝗞𝗜𝗞𝗔 90 𝗭𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗭𝗜𝗠𝗘𝗜𝗦𝗛𝗔
:
Dakika 90 za kwanza Kocha Nasserdine Nabi amefeli kwenye Selection ya Team na kwenye SUB Alifeli kwa 95%
KIVIPI
••••••••
1. Adeyun Salehe:- Sijajua aliyependekeza kubaki kwake, hasitaili kuchezea Club yanga na Hakuna mjadala.
:
2. Zawadi Mauya:- Mpaka Dirisha linafungwa sijajua alibakia Yanga kufanya Nini! Anaidhalilisha Nembo ya Yanga anachokifanya ni upumbavu mtupu uwanjani, kama angekua na mkataba angerudi tu Kagera akazeekee kule.
:
3. Kocha naona kibarua kitamuozea mapema sana, Unamuachaje mtu kama Saido,Bangala,Kaseke wakae Benchi ilihali Timu inazidiwa??
:
4. Kibwana Shomari anataka kuiga Uchezaji wa Djuma Shabani, Kwanini usicheze kwa style yako uliyoizoea??
:
5. Sijajua Kinachomuweka Nje David Bryson mpaka Leo hii, kama hana Match fitness alisajiliwa ili atumike lini?? Madactari wanafanya kitu Gani mpaka Leo hii!!
Hakuna kitu wanachokosewa wanayanga kama mambo yanayoendelea sasa, Picking ya Coach inaanza kufeli mapema....
Team Kushinda ni Jukumu lenu na kulaumiwa hatuachi mpaka mjue Mmebeba furaha ya wananchi wangapi, Haiwezekani Mtu unalipwa vizuri, unakula vizuri, Unalala pazuri alafu unachofanya uwanjani ni Utumbo wa mbwa kabisa
:
Atakaesema Lawama za Nini kwanini tusiwalaumu wakati walisajiliwa waje waitumikie Team yetu kwa jasho na damu!
:
Atakaeleta Masihara naomba Uongozi usiwachekee ni kufukuza tu wakafanye shughuli walizozaliwa nazo
 
Uto hawabebeki [emoji38]
Screenshot_20210912-202227_1.jpg
 
Yanga ilijiandaa kwa ajili ya Tamasha la utambulisho wa wachezaji na Haji Manara tu.

Haikuiandaa timu kwa ajili ya ushindani wa michezo ya CAF. Bado haina ubavu wa kufanya vizuri. Wachezaji wote ni wazuri ila bado wataishia kucheza vizuri dakika 45 tu. Mpaka mje mkae sawa mtakuwa mshachelewa.
Mkuuu kauli yako imejidhihirisha waz waz hongera kwa kuujua mpira
 
Back
Top Bottom