Yanga ina matatizo makubwa kimataifa

Analysis nzuri isipokuwa kwenye ball control Kwa Wachezaji wa mbele. Mayele na Ki ni ball holders Kwa hiyo hujawatendea haki kuwaweka kapu moja na Kisinda na Moloko.
Sina hakika km umewafuatilia vizuri. Mayele ni mfungaji mzuri lakini anapoteza sana mpira kirahisi. Nakuomba umfatilie Jumapili na Mazembe. Aziz ki naomba na yeye umfatilie utaungana na mimi.
 
Wakati nikikubaliana na hoja zako kwa asilimia kubwa, nina swali kwenye yako ya kwanza. Kwenye hiyo hoja umesisitiza umuhimu wa wachezaji wenye maumbo makubwa.

Swali ni inakuwaje nchi zenye wachezaji wasio na maumbo makubwa kama Japan na Korea Kusini zinaweza kupata matokeo dhidi ya giants kama Cameron na Ujerumani ?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Sina hakika km umewafuatilia vizuri. Mayele ni mfungaji mzuri lakini anapoteza sana mpira kirahisi. Nakuomba umfatilie Jumapili na Mazembe. Aziz ki naomba na yeye umfatilie utaungana na mimi.
Naongea nikiwa nimewaona na kuwafuatilia Sana. Mayele ana uwezo mkubwa wa kuhold mpira, sema Kwa vile yeye ndo last man anawahi kuachia ili akakae sehemu yake na hapo ndo anakosa Nani ampokee majukumu. Jana umeona tofauti alipokuwa Peke yake na alipoingia Musonda?
 
Simba sasa mmekuwa wachambuzi wa kikosi cha Yanga mnasahau juzi mmepigwa. Kwa Yanga hii ndio ilikuwa mechi ngumu kuliko zote, ni sawa na Raja wanavyowasubiri nyumbani.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Ya juzi tumeyasahau tena wala hayatuumizi

Kwani we yale maneno mliyokuwa mnatutolea juzi hujayasahau?

Hao Raja sijui kina Roja waache waje ila hapa Lupaso haiwezi kuwa simple kwao hata siku moja
 
Mbinu tu za uchezaji.....
 
Mbinu tu za uchezaji.....
Unapokuwa na wachezaji wafupi kuna vitu makocha huwa wasisitiza kwa wachezaji wake.
1. Kuepuka kufanya faulo maeneo ya hatari.
2. Kuepuka mipira ya kona.
3. Kufanya taiti markings.

Km unakumbuka ile Barcelona ya kina Xhavi,Iniesta na Messi walikuwa wanakwepa sana kona au faulo kwenye eneo lao,muda mwingi walikuwa wanamiliki wao mpira. Wakipoteza ndani ya sekunde chache wanaurudisha kwenye himaya yao. Tujiulize je sisi tuna hao wachezaji wafupi na mafundi km kina Xhavi na Iniesta wa kuwafanya timu pinzani wateseke ndani ya uwanja? Kwa sababu ukiwa na wachezaji wafupi silaha kubwa ni kumiliki mpira,akili nyingi na nidhamu kubwa.
 
Kwa maana hii unasema tatizo siyo vimo vya wachezaji ila mbinu za mwalimu?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo namba 7 ukweli mtupu 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…