Yanga inapata faida kweli kucheza ligi kuu tu, huku kimataifa hawapo?

Yanga inapata faida kweli kucheza ligi kuu tu, huku kimataifa hawapo?

Tangu simba wameanza kucheza kimataifa wamepata mafanikio gani hata makao makuu hawana?
na wewe ni mmoja wao kama asemavyo msukule pale utopoloni?

B9B4FC43-83F3-4F82-A5E0-74FDC512CA43.jpeg
 
Inayocheza kimataifa haina uwanja wake hadhi ya azam hivyo wanaocheza kimataifa nao hasara tu
 
Yanga ni club inaayoendeshwa kwa hasara 99% maana hawafanyi hata biashara ya kuuza wachezaji huwa hawanunuliwi na club zingine ila huwa wanaondoka bure baada ya mkataba kuisha
Nafikiri ni watu wachache tu wenye pesa zao wameamua kuifadhili lakin hakuna faida yoyote wanayopata
Hivi simba inaendeshwa kwa faida?? Mudi mara kibao analalamika kupata hasara! Upo nchi mzee?? Mliuza garasa lenu kule Morocco limekaa wiki 6 tu, limerudi kucheza na kina Dar city!
 
Wametumia kiasi gani kwenye mashindano hayo yaliyowapa 3.8bn?
Nauli, kambi, hotels etc..
mpe ilimi ya msingi ya biashara.
mapato - matumizi = Faida

Ndugu yetu mapato anaita Faida dah!!!
Mtu huyu kujiajiri hatoweza, atafutiwe tu kibarua.
 
Sina exact figure lakini kwenye bajeti yao ya mwaka kila unapoingia kwenye hatua nyingine inakuwa ni msaada wa kupunguza matumizi yaliyokusudiwa.
Kuna timu zilishiriki na kuondolewa bila kupata chochote licha ya kuingia gharama.Kuna timu hata ilikosa nauli ya kwenda Libya.
Kipato chochote unachopata extra is a bonus regardless ya matumizi uliyo
kwisha panga.
Ukiangalia kwa angle ya ushabiki mimi sipo huko.
Wewe umeangalia kwenye angle ya ushabiki.
Kama cost = revenue basi hamna faida ni sawa na neutral hamna tofauti kati ya mshiriki na asiyeshiriki kimapato.
Kama cost > revenue basi ni hasara kushiriki hayo mashindano.
Kama cost < revenue basi ni faida kushiriki hayo mashindano.

FYI ni zaidi ya 50,000$ to 100,000$ gharama ya mechi ya kombe la Africa. Thats the cheapest, kwa timu kubwa ni zaidi kwa sababu allowances za michezo hiyo ni kubwa kwa wachezaji na bench.
Ndiyo maana sometimes kwa timu ndogo ni hasara tu kushiriki Caf, lazima uwe na budget kubwa.
 
Subiri Yanga tuchukuwe kombe letu halafu mwaka huu tuingie kwenye club bingwa na hiki kikosi cha akina Mayele ndo ataona moto wetu..
Mwakani lazima tufike Nusu Fainali Championship
 
Subiri Yanga tuchukuwe kombe letu halafu mwaka huu tuingie kwenye club bingwa na hiki kikosi cha akina Mayele ndo ataona moto wetu..
Mwakani lazima tufike Nusu Fainali Championship
Labda kombe la mbuzi.
 
Kwahyo na hili kombe tunaloenda kunyanyua kwapa tarehe 30 April baada ya kuwapakuwa pale kwa Mkapa litakuwa kombe la mbuzi ety..
Labda kombe la mbuzi.
Maana Sasa mnatumia Hadi uchawi kutaka mtushushe kileleni Ila hamuwezi.
Sisi ndo Mabingwa mara nyingi wa nchi hii
 
Moja kati ya nguzo kuu za mpira wa sasa ni kucheza mashindano ambayo yatakuwa yanaisaidia club kujiendesha pasipo kutegemea sana kupitisha mabakuli kwa matajiri na wadhamini ndio maana ulaya kocha anaweza akafukuzwa sababu ya kutolewa uefa kizembe au kutofuzu kabisa huwa inachukuliwa kama hasara kubwa kwa timu.

Kwa muda mrefu yanga wamefocus sana kwenye makombe ya ndani ambayo hayana pesa wala faida ya maana, ligi kuu ukichukua ubingwa ile pesa wanayolipwa kama zawadi unaweza kuta ni mshahara wa mayele tu wa miezi kadhaa sasa hebu fikiria club nzima itajiendeshaje kwa pesa ile maana ni ndogo sana

Nilitegemea yanga kwa kikosi kile now ingekuwa robo fainal CAF maana naona ligi ya ndani wapo vizuri sana ila CAF kama kuna pepo sijui maana kila yanga ikinusa CAF basi makundi ndio mwisho wao

Ila CAF kuna pesa, simba ilipovuka robo fainali mara kwa mara walikuwa wakipata bilioni 1 na ushee na juzi naskia wamepata milioni 800

Tukubali ukweli Yanga inahitaji kujiongeza sana kwenye mashindano ya kimataifa maana ligi za ndani mtaishia kuendesha Club kwa majashoo ya wadhamini na masponsa wa Gsm wakati kile kikosi kina uwezo wa kupambana kimataifa na mkachota pesa ndefu ambayo itasaidia kwenye uendeshaji wa Club

Najua mtakuja kuniita makolo ila timu inatakiwa ibadilike sana maana mnapata wachezaji wazuri lakini hamuwatumii vizuri kimataifa wawaingizie pesa, Mtu kama mayele mnaweza mkawa nae msimu na msimu ujao matajiri wakampandia dau akaondoka na ukiangalia mmemtumia vyema ligi ya ndani tu kimataifa hampo.
Yaani umejipinda kuleta hoja utafikiri timu ya Simba imeundwa mwaka 2019 vile. Anza kuhoji kwanza timu yako je wakiachana na miaka ambao inahesabika kwa kufika robo michuano ya kimataifa. Je kipindi ambacho hawakufika huko hawakusajili? Je usajili waliofanya umewapa vipi faida?

Jambo lingine la ziada tu ni kwamba ni kwanzia msimu huu ndio tutashuhudia bingwa wa ligi kuu akupokea 0.5 billion wakati zamani tulishuhudia timu pamoja na kutumia gharama kubwa za kuandaa timu na kujiendesha kucheza mechi lakini zawadi ni milioni 80 tu
 
Simba ilifika nusu fainali ya Klabu bingwa ya Afrika mwaka 1974.
Na ikafika tena fainali ya kombe la Wawakilishi 1993.
Kwa hiyo usifikiri mafanikio hayo yameanza 2019.
Au umeanza kufuatilia mpira 2019?
 
Kwahyo na hili kombe tunaloenda kunyanyua kwapa tarehe 30 April baada ya kuwapakuwa pale kwa Mkapa litakuwa kombe la mbuzi ety..

Maana Sasa mnatumia Hadi uchawi kutaka mtushushe kileleni Ila hamuwezi.
Sisi ndo Mabingwa mara nyingi wa nchi hii
Hizo ngonjera za sisi mabingwa wa mara nyingi halafu mnafaidika nini?Kupigwa nje ndani na timu mbovu kama Rivers United ndio cha kujivunia?
Miaka mnayochukua ubingwa na kuwakilisha Nchi mnaiishia kutia aibu Nchi.
 
Yanga ni club inaayoendeshwa kwa hasara 99% maana hawafanyi hata biashara ya kuuza wachezaji huwa hawanunuliwi na club zingine ila huwa wanaondoka bure baada ya mkataba kuisha
Nafikiri ni watu wachache tu wenye pesa zao wameamua kuifadhili lakin hakuna faida yoyote wanayopata
Watakupiga mawe
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hizo ngonjera za sisi mabingwa wa mara nyingi halafu mnafaidika nini?Kupigwa nje ndani na timu mbovu kama Rivers United ndio cha kujivunia?
Miaka mnayochukua ubingwa na kuwakilisha Nchi mnaiishia kutia aibu Nchi.
Narudia tena SS ni Mabingwa mara nyingi Tz hii hakuna lol ikolonlolote Lina Lowes kutufikia SS kwa ubingwa na Mwaka huu tar 30 April tunaenda kutangaza ubingwa mwingine mgongoni kwa Makolo FC a.k.a Manyaunyau FC.. ss ndio wanaume wa nchi hii hakuna mwingine,, tunaenda kuwafunga Makolo Timu ambayo tumeifunga maraaaaaaaaa nyiiiiiiiiiiiiiiingi kuliko Timu yoyote Dunia hii
 
Simba ilifika nusu fainali ya Klabu bingwa ya Afrika mwaka 1974.
Na ikafika tena fainali ya kombe la Wawakilishi 1993.
Kwa hiyo usifikiri mafanikio hayo yameanza 2019.
Au umeanza kufuatilia mpira 2019?
Yanga hawajawahi kumiliki akili.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom