Yanga itaenda kuvunja rekodi zote zilizowekwa na Simba kimataifa

Yanga itaenda kuvunja rekodi zote zilizowekwa na Simba kimataifa

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Ukitazama kwa jicho la kimpira utakubaliana na mimi ya kuwa klabu ya Yanga itafika mbali zaidi ya ilipofikia Simba kwenye michuano hii ya CAF.

Ikumbukwe Yanga inashiriki kombe la shirikisho Afrika ambalo mwaka jana Simba alifika robo fainali, ila hakuna klabu yoyote nchini iliyowahi kuvuka nusu fainali iwe klabu bingwa au kombe la shirikisho ambalo limeanzishwa na caf mwaka 2004.

Hivyo tusishangae tukiona Yanga ikichukua kombe hili la shirikisho na kuiletea nchi yetu heshima kubwa.

yangasc_1674787135685915.jpg
 
Mimi ni mwananchi halisi lakini sioni aibu kusema Simba ilishafika fainali ya kombe la shirikisho na kupoteza Kwa Stella Artois1993. Mchezo ulichezwa Kwa siku mbili. Wenye kumbukumbu nzuri tukumbusheni
 
Mimi ni mwananchi halisi lakini sioni aibu kusema Simba ilishafika fainali ya kombe la shirikisho na kupoteza Kwa Stella Artois1993.
Mchezo ulichezwa Kwa siku mbili.
Wenye kumbukumbu nzuri tukumbusheni
Mkuu hilo halikuwa kombe la shirikisho, hebu pitia vyanzo vyako vya taarifa tena
 
Acha uongo na rekodi za mchongo, yaani unataka kufuta rekodi za Simba kirahisi hivyo?
1. Simba ilifika hatua ya Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993
2. Simba ilifika hatua ya Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974


View attachment 2544038
Kwaio hicho kipande cha karatasi ndio kina justify hoja Yako? Nikisema hivi nawewe utaamini?
JamiiForums1522568394.jpg
 
Kwaio hicho kipande cha karatasi ndio kina justify hoja Yako? Nikisema hivi nawewe utaamini?
Mbona unarukaruka, si usimame kwenye hoja ya uzi wako kwamba Yanga ndio itakuwa timu ya kwanza Tanzania kwenye michuano ya Afrika kufika Nusu Fainali? Usiukimbie uzi wako, endelea hivyo hivyo. Ndio mkome kuanzisha nyuzi wakati hamna data
 
Waulize CAF. Tena usiishie hapo, waulize kwa nini wameichagua icheze Super League kabla ligi ya NBC haijaisha, bila kujali itashuka daraja au la
Hahahahaha... Ilo haliondoi ukweli Yanga imeinuka na ni suala la muda tu heshima yake itatambulika Afrika sio kwa kufika tu robo fainali bali kwa kuwa mshindani wa vikombe barani Afrika.
 
Back
Top Bottom