SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Yanga wamefanya kosa kubwa kwenye mkataba wao na SportPesa kuliko wengi tunavyodhani na madhara yake ni makubwa sana kwa mdhamini wao yaani SportPesa. Yaani mimi ningekuwa mshabiki wa Yanga ningemtafuta huyu aliyetoa wazo hili maana ni msaliti mkubwa sana atakayeenda kuiharibia timu si tu kibiashara na kifedha lakini pia focus kwenye mechi zinazofuata.
Athari ya walichofanya Yanga ni kubwa kwa sababu hata ikitokea leo Yanga wakaghairi kutovaa jezi hizi mpya katika mechi zao za CAF Shirikisho, jezi hizi tayari zipo mtaani na watu wanazivaa zaidi ya zile za zamani kwa wale waliokuwa na uwezo wa kuzinunua.
Hawa SportPesa wakikomaa wakasema wamesamehe hawataidai fidia au kuvunja mkataba, watakachotaka kufanya the least ni kuitaka Yanga kuzinunua jezi zote walizouza ili kuziondoa mitaani. Na tunajua wakisema wazinunue kwa bei ile ile waliyouzia mwanzo, wachache sana watarudisha.
Hivyo Yanga itabidi waweke bei kuanzia 80,000/= kwa kila jezi ndiyo labla itawashawishi watu kuzirudisha.
Mgogoro mkubwa unanukia Yanga.