Yanga kimeumana, hatimaye tumeanza kunena lugha moja

Yanga kimeumana, hatimaye tumeanza kunena lugha moja

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
 
Attachments

  • 20210228_07255593068.mp4
    2.6 MB
  • 20210228_07250215388.mp4
    1.1 MB
  • 20210228_071827177410.mp4
    2.1 MB
Yanga wameshinda lakini hawana furaha. 🤣🤣🤣🤣
 
hakuna cha kuumana ni kuingia na matokeo yao kwani keni gold sio timu hadi uipige 8 huko epl man u kapigwa na timu ya mwisho kwenye ligi nyau alitolewaga na timu ya jeshi daraja kwa kwanza mwaka juzi (nimewasahau jina )

nafikiri ni uchanga wa kujua mpira na kuingia na matokeo yao mkononi kwamba ukamfunge ken gold 10 kwani hao wa yanga mpira wanapiga kwa kutumia ulimi,ama mikono wote wanatumia miguu ni kawaida.
 
Bora Yanga kashinda goli moja, Nyau walipigwa na Green city pamoja na Green worriors! Bora! Ni kweli hakuna timu ndogo ktk soka!
 
Utopolo mtupu wanaongea huku Sibomana anawadai, Tambwe anawadai tatizo lao kubwa wanataka kushindana na mnyama wakati sio level yake
 
Shida kubwa ya mashabiki wa Yanga hawajui tatizo la timu yao lipo wapi. Walianza kuilaumu TFF na kamati zake zote, waamuzi, baadhi ya viongozi wa serikali na Simba kuwa wanaihujumu timu yao wakati si kweli. Sasa wamehamia kuulaumu uongozi wa timu yao na muda sio mrefu watawalaumu wafadhili wao.

Ukweli mchungu sana kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa benchi lao la ufundi lina tatizo kubwa sana. Pamoja na usajili mbovu uliofanyika kwenye dirisha kubwa na dogo lakini tatizo lipo kwenye upangaji wa timu kwani kuna baadhi ya wachezaji wapo vizuri sana. Ni maajabu ya mwaka kila siku unampanga Sarpong na Nchimbi kila mechi halafu unamuweka Wazir Junior benchi mwenye magoli 8+ katika ligi iliyoisha halafu unategemea upate ushindi. Huyo Wazir Junior mpe mechi 5 mfululizo kwanza azoee presha za timu kubwa kama Yanga halafu utaniambia moto wake. Huyo Sarpong kila siku anakosa magoli ambayo hata ukimchukua fowadi wa Yanga Princess anafunga.

Kibaya zaidi kwa Yanga ni kumuacha Mwambusi aondoke halafu unamleta Nizar Halfan kwenye nafasi yake. Nizar hana uzoefu wa kutosha kwenye ufundishaji zaidi tu ya kucheza kwenye ligi. Kama Yanga wangekuwa makini walipaswa wawe na kocha msaidizi mwenye ujuzi na uzoefu wa ligi kuu bara kama Mexime au Mbwana Makata. Mfano mzuri ni Simba kocha wao msaidizi ni Matola ambaye amecheza ligi kuu bara na amewahi kufundisha timu za ligi kuu bara kwa mafanikio kiasi fulani kwa hiyo anajua mazingira yote ya ligi kuanzia viwanja mpaka mifumo ya uchezaji ya kila timu. Pia kwa haraka sana kuwe na kamati ya ufundi yenye iundwe na watu kama wakina Ali Mayi, Sekiloja Chambua na wengineo kwa ajili ya kulishauri benchi la fundi mara kwa mara.

Yanga bado wana nafasi ya kufanya vizuri tu iwapo kwanza wataaacha kumalumu kila mtu kwa matokeo ya mabovu badala yake waimarishe benchi lao la ufundi kwa kumletea Kaze kocha msaidizi mzawa mwenye uzoefu ligi yetu na pili kupanga vizuri timu yao kwani baadhi ya wachezaji wao wazawa wana uwezo kuliko wageni lakini hawapewi nafasi ya kutosha kuonyesha uwezo wao.
 
hakuna cha kuumana ni kuingia na matokeo yao kwani keni gold sio timu hadi uipige 8 huko epl man u kapigwa na timu ya mwisho kwenye ligi nyau alitolewaga na timu ya jeshi daraja kwa kwanza mwaka juzi (nimewasahau jina )

nafikiri ni uchanga wa kujua mpira na kuingia na matokeo yao mkononi kwamba ukamfunge ken gold 10 kwani hao wa yanga mpira wanapiga kwa kutumia ulimi,ama mikono wote wanatumia miguu ni kawaida.
Mpira ume igiliwa na wapuuzi kulalamika tu kila kitu wakati hata maisha yao wame fail, ile game Ilikua ya knock out hai hitaji mambo mengi lkn mijitu bado ina lalama, ingekuaje wangefungwa?
 
Mpira ume igiliwa na wapuuzi kulalamika tu kila kitu wakati hata maisha yao wame fail, ile game Ilikua ya knock out hai hitaji mambo mengi lkn mijitu bado ina lalama, ingekuaje wangefungwa?
umesha sema ni knock out ikiwa wangefungwa bas ndo kwisha habari yao simba alitolewa na gree worious ni soko mkuu.

sema wachezaji wa yanga wanazingua sana.
 
Wapigane pale Jangwani tuone hasura zao kwa kumaanisha.
 
Kuna ukweli
FB_IMG_1614600244576.jpeg
 
Kocha msaidizi si ana dread?Ndio chaguo la utopolo.Wakiona pia mchezaji ana dread wanasajili.Sarpong ni jina linalotumika kutishia tu kwani utopolo ni watu wa maneno.Sar-ponG! Ina sound kama shuti kali!Hawa uto akili yao wanaijua wenyewe
 
Back
Top Bottom