Yanga kufika nusu fainali Klabu Bingwa Afrika 2022/23?

Yanga kufika nusu fainali Klabu Bingwa Afrika 2022/23?

Mechi ya kwanza tu mnapangiwa na timu za uarabuni na safari yenu inaishia hapo. Poleni sana. Asanteni kwa kuja
 
Mbona fainali aliyocheza Simba dhidi ya stella abdjan hujaweka kama ni deni kwa utopolo?
kwanza fainali na stella haikuwa klabu bingwa, ilikuwa ni fainali ya kikombe kimoja kilichozuka miaka ya 1990's kiliitwa CAF CUP, Caf Cup ilizidiwa hadhi na klabu bingwa na kombe la washindi barani afrika na pia haikuwa 1974 hebu soma makala kwa makini
 
kwanza fainali na stella haikuwa klabu bingwa, ilikuwa ni fainali ya kikombe kimoja kilichozuka miaka ya 1990's kiliitwa CAF CUP, Caf Cup ilizidiwa hadhi na klabu bingwa na kombe la washindi barani afrika na pia haikuwa 1974 hebu soma makala kwa makini
 
YANGA KUFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA 2022/23?

Mwaka 1974 Klabu ya soka ya Simba ilipewa jukumu la kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Simba ambao walipata tiketi hiyo baada ya kutwaa ubingwa mwaka 1973 walijikuta wakiwa na deni kubwa kwa vile watani zao Yanga walikuwa wamefanya mambo makubwa yafuatayo:

Kwanza Yanga walikuwa wamechukua ubingwa wa Tanzania mara tano mfululizo (1968,69,70,71 na 72)

Pili walikuwa wametinga na robo fainali mbili za klabu bingwa (1969 na 1970) robo fainali ambazo zote Yanga ambazo zote mbili Yanga ilijikuta ikicheza na Asante kotoko ambao ndiyo waliochukua ubingwa wa afrika (1970)

Hata hivyo Simba hawakutishwa na rekodi za Yanga waliingia mashindanoni na kwenda moja kwa moja hadi nusu fainali ambapo walitolewa kwa matuta na Mehalla Al-Kubra ya Misri kwa lugha nyingine Simba walilipa deni na kuweka rekodi mpya.

Mwaka huu (2022/23) Yanga inaingia kwenye mashindano ya klabu bingwa wakiwa na deni kubwa kwa watani zao ambao nao wamefanya yafuatayo:

Kwanza wamechukua ubingwa Tanzania mara nne(04) mfululizo

Pili wameingia robo fainali mbili za klabu bingwa(2019 na 2020/21) Katika robo fainali mojawapo Simba imetolewa kwa matuta na Orlando Pirates wakati Robo fainali nyingine Kaizer Chiefs waliomba mpira uishe. Pia wameingia robo fainali ya kombe la shirikisho

Je, Yanga atafanya alichokifanya mtani wake mwaka 1974 kwa kulipa deni na kuweka rekodi mpya? Yetu macho.
Kufika nusu fainali siyo matako kuwa kila mtu anayo.
 
Back
Top Bottom