Yanga Kukosa Magoli Ushirikina Unatumika

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Wengi hawataamini lakini ukweli ndio huu,
Hali ya kukosa mabao kwa Yanga leo imeingia katika mechi dhidi ya Tanzania Prison, kabla ya hapo zimekuwepo mechi kadhaa ambapo Yanga mbali ya kucheza vizuri na kupata nafasi mipira imekua haiingii golini,

Tukianza na mchezo baina ya Yanga na Simba washambuliaji wa Yanga wameshindwa nafasi za wazi kabisa kuingiza mpira wavuni, Mfano zile chance za Denis Nkane

Mechi na Jkt Ruvu pale Kigoma pia goli lilionekana zito mpira kuvuka na kuingia ndani ya nyavu, ikumbukwe siku ile Jesus Moroco alikosa nafasi mbili tatu za wazi,Fiston Mayele aligongesha bomba mara mbili na nafasi nyingine mpira alioupiga ukaenda nyavu ndogo

Mechi hii na Prison Mayele anashindwa kufunga nafasi za wazi ikiwemo penati, Faisal naye..Makambo eti anashindwa kuusukumia ndani mpira japo kwa kuugusa tu!

Ukichukulia ki kawaida utaona labda ni kawaida lakini ukifikiri deep utagundua hapo kuna mikono ya kishirikina tu ambapoo kuna watu ama kikundi cha watu hawapendi na hawataki Yanga iendelee kushinda game zake zilizobaki
Mayele si wa kiwango hicho na hili linajulikana.Yaani hadi unaona wachezaji wanapigwa butwaa!

Ila tunasema mwisho wa siku mchawi atajulikana.
 
HAPANA nakataa kabisa..! Kuna wakati game hukataa tuu hasa kutokana na kupania sana ama kudharau, uchovu , hali ya hewa nk nk
Hiyo ni hali ya kawaida hakuna juju hapo..

Hizo situation hutokea popote kwenye michezo mingine kama boxing. Mbio nknk.. Huweza kutokea pia kwenye mitihani interview na hata kwenye mahusiano kipengele cha ngono, nknk

Hata viwandani wale walio kwenye production line wanatambua hilo.. Kuna siku mtambo wa line fulani huwa mzito bila sababu wakati ndio unaoaminika kwa kupiga kazi.

Hata kwa madereva pia kuna wakati unakanyaga mafuta lakini speed haibadiliki.. Hili jambo ni la kiroho zaidi kuliko imani na hisia za ushirikina
 
Utopolo kweli ni utopolo. Yaani unahalalisha ukilaza wa wachezaji kuwa wamelogwa.
 
Wengi hawataamini lakini ukweli ndio huu,
Hali ya kukosa mabao kwa Yanga leo imeingia katika mechi dhidi ya Tanzania Prison,kabla ya hapo zimekuwepo mechi kadhaa ambapo Yanga mbali ya kucheza vizuri na kupata nafasi mipira imekua haiingii golini...
Hakuna uchawi bahati haikuwa yetu
 
Huyu mchawi na aendelee kuwaroga mpaka mwisho wa ligi. Maana itakuwa manara ameshindwa kuwasaidia.

Wachawi kwa wachawi wanajuana.

Ingekuwa uchawi unacheza basi Timu za Bamoyo, Tanga au Sumbawanga kwa mfano zingekuwa ligi kuu na kutwaa kombe la dunia.

Tuondoleeni huu ujinga chezeni mpira
 
On target 5 off target 2,kule kigoma ilikua ikipigwa inagonga mwamba inarudi,watu wanamkomesha mayele baada ya kudai ana deni na namungo na makolo,ile kitu makolo imewauma sana wanakomesha,ile penalti mpira hata ulivyopaa juu 😀

 
Mwafrica anawaza ngono&uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…