kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Katika fani ya magonjwa ya akili yapo magonjwa kama vile msongo wa mawazo (stresses) na sonona (depression) ambayo tiba yake kuu ni kutoa ya moyoni hadharani au kwa mtu unaemwamini. Tiba hii kitaalam inaitwa "mental ventilation" au mental catharsis. Unapokuwa unaongoza watu hakikisha kuwa unafanya vikao vya mara kwa mara na watu wako na uwape muda wa kutosha watoe madukuduku yao kuhusu kazi, maisha na mahusiano kazini. Hii itasaidia kuimarisha afya ya watu wako na ufanisi kazini.
Jemedari anaiandama Yanga sio kwa bahati mbaya tu, nadhani anaumwa (tresses au sonona) kutokana na mambo yenye uhusiano na Yanga. Inawezekana anayo malalamiko ambayo hayatimizwi au hayakutimizwa huko nyuma ambayo yalimuudhi, yalimtia hasara au yalimuaibisha yanayohusiana na Yanga. Hivyo anakabiliana nayo kwa kuisema yanga kama sehemu ya tiba; mental ventilation (kujijambia jiwe).
Tiba yake hii itakamilika kama akiona Yanga wanahangaika na ventilation anayoifanya kila siku. Ili kumuongezea mauvumivu ni kuacha kuhangaika na kumjibu kila anachosema, badala yake ongezeni juhudi uwanjani matokeo ya Yanga yawe mazuri kila siku. Maana mtu unaemhisi anatembea na mkeo (mbaya wako) hupendi achaguliwe kuwa diwani (hupendi afanikiwe).
Kuendelea kumjibu ni kunasa kwenye mtego wake.