Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
NYOTA KADHAA WA KIMATAIFA YANGA WATAIKOSA FAINALI TANGA, Klabu ya Yanga itawakosa Fiston Mayele na Stephen Aziz Ki ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa kuelekea kalenda ya FIFA, huku wakiwa wameondoka mapema leo kwenda kwenye majukumu yao.
Kama hivyo haitoshi Yanga ilipambana kuhakikisha angalau Djigui Diarra wa Mali, Kennedy Musonda wa Zambia na Khalid Aucho wa Uganda waweze kusalia kambini kucheza fainali ila nao imeshindikana kwa Diarra na Musonda kwakuwa Mashirikisho yao yamekaza ni Uganda pekee wameridhia Aucho aripoti baada ya fainali kwakuwa sio mbali. Kwanini imetokea hivyo?
Ni kuwa fainali ya FA CUP imepangwa muda ambao kalenda ya FIFA inaanza, huku inafahamika kuwa wachezaji walioitwa timu zao za taifa ni mali ya Federation hivyo kutoripoti mapema kambini ni kosa ambalo Mchezaji anaweza kukumbana na adhabu, huku kwenye kalenda rasmi huu ni wakati wa mechi za Kimataifa.
Mpaka hivi sasa Mali na Zambia tayari wametuma tiketi kwa Wachezaji wao na wanahitaji waliripoti kabla leo haijapita kambini, nje na hapo Yanga wamepewa taarifa Wachezaji hawatopokelewa na adhabu stahiki zitachukuliwa kwa Wachezaji. Maswali kichwani mwa Yanga mpaka hivi sasa ni je?
Yanga watakaidi amri na kuwatumia wachezaji hao kesho na kupokea adhabu? Ndicho kinasubiriwa mpaka hivi sasa, chanzo changu bado hakijapata maamuzi ya mwisho ya Yanga. Hizi ni taarifa ambazo nimezipata kutoka kwa vyanzo vyangu hivyo uwezekano ni rotation kubwa ya kikosi kwa Yanga hapo kesho.