Michezo/Mpira sasa hivi ni biashara Chifu..Kituo cha Luninga kinachotaka kuonesha mechi ya Yanga kinapaswa kuwalipa Yanga fedha kwa ajili ya matangazo hayo...
Hakuna cha bure sasa hivi...Hata wewe usipolipia Azam TV hauwezi kuwa na access ya Azam 1 au 2 zinazoonesha mpira...Ni lazima ulipie kwanza ndo uangalie hizo channel...Hata Super Sport na Sky Sports ni hivo hivo..
Timu za ligi kubwa kama RMA na Arsenal zinaingiza fedha nyingi kutokana na malipo ya haki za matangazo ya moja kwa moja ya luninga...
Kabla haujaanza kuilalamikia Yanga jaribu kuuliza endapo kituo chochote cha Luninga kilijaribu kuingia makubaliano na Yanga juu ya kununua haki za matangazo hayo...Na ujue kama walishindwana ama la...
Vituo vya luninga vinapata fedha nyingi na faida kubwa kutokana na udhamini wa makampuni katika matangazo ya moja kwa moja....
Inabidi tubadilike na kuona kwamba mpira wa sasa ni biashara...Hawa akina Niyonzima..Tambwe..Coutinho et al wanahitaji kulipwa fedha nyingi tu...Hizi si zama za bure Chifu...Hasa kwenye mashindano makubwa kama confederation cup...
Mpira ni pesa na TV stations zinapaswa kubadilika..Ndo maana Azam TV wanatoa zaidi ya Tshs. Milioni 100 kwa kila timu inayoshiriki VPL kama sehemu ya gharama za udhamini kutokana na haki za matangazo..
Jiulize ni kwa nini Azam TV wamenunua haki za matangazo za VPL?...
Hauoni kwamba kwa Yanga kuruhusu Azam TV waoneshe bure mechi itakuwa ni kuifaidisha Azam TV kutokana na sababu kwamba Azam TV watafaidika na fedha za malipo/gharama za kulipia kuona Azam 1 na 2 pamoja na udhamini wa matangazo hayo ya moja kwa moja(matangazo ya biashara ya bidhaa za SSB)...