Yanga: Mechi yetu na Etoile du Sahel haitaonyeshwa runingani

Yanga: Mechi yetu na Etoile du Sahel haitaonyeshwa runingani

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Klabu ya Yanga imeyasema hayo leo.

Kimsingi,huo ni mgando wa fikra na hoja. Hakuna sababu za kufanya hivyo. Kuonyweshwa ni kujitangaza zaidi na kuwasaidia watanzania waliombali na Dar kujionea timu yao.

Nikiwa mshabiki wa Yanga,napinga kusudio hilo na kuliona halina maana. Mambo hayo ni ya kizamaní. Yanga mfikirie na kuamua tena kabla ya Jumamosi
 
Ha...hawa jamaa wamerudi tena kutokutuonesha huu mtanange...hii ni kutokuwatendea haki wapenzi na mashabiki wa mpira ambao kwa sababu yoyote ile hawataweza kufika uwanjani!!
 
Kama hawato onyesha naombea yanga ifungwe 3-0. Ila wakionyesha naombea yanga ishinde 2-0
 
Mleta mada kuwa specific ktk habari yako.je unamaanisha mechi zote mbili?au ni moja tu ya hapa taifa?KM NI 1 CO TATIZO SN
 
Ni mechi ya taifa pekee haitaoneshwa ila ya marudiano azam wataonesha....




Wahindi wamekutana lazima watunishiane kila moja anayo pesa


Ijumaa naja taratibu dar kuangalia mtanange MUNGU epusha ajali za barabarani

Daima mbele
 
Yanga wanaanza kutuboa

Michezo/Mpira sasa hivi ni biashara Chifu..Kituo cha Luninga kinachotaka kuonesha mechi ya Yanga kinapaswa kuwalipa Yanga fedha kwa ajili ya matangazo hayo...

Hakuna cha bure sasa hivi...Hata wewe usipolipia Azam TV hauwezi kuwa na access ya Azam 1 au 2 zinazoonesha mpira...Ni lazima ulipie kwanza ndo uangalie hizo channel...Hata Super Sport na Sky Sports ni hivo hivo..

Timu za ligi kubwa kama RMA na Arsenal zinaingiza fedha nyingi kutokana na malipo ya haki za matangazo ya moja kwa moja ya luninga...

Kabla haujaanza kuilalamikia Yanga jaribu kuuliza endapo kituo chochote cha Luninga kilijaribu kuingia makubaliano na Yanga juu ya kununua haki za matangazo hayo...Na ujue kama walishindwana ama la...

Vituo vya luninga vinapata fedha nyingi na faida kubwa kutokana na udhamini wa makampuni katika matangazo ya moja kwa moja....

Inabidi tubadilike na kuona kwamba mpira wa sasa ni biashara...Hawa akina Niyonzima..Tambwe..Coutinho et al wanahitaji kulipwa fedha nyingi tu...Hizi si zama za bure Chifu...Hasa kwenye mashindano makubwa kama confederation cup...

Mpira ni pesa na TV stations zinapaswa kubadilika..Ndo maana Azam TV wanatoa zaidi ya Tshs. Milioni 100 kwa kila timu inayoshiriki VPL kama sehemu ya gharama za udhamini kutokana na haki za matangazo..

Jiulize ni kwa nini Azam TV wamenunua haki za matangazo za VPL?...

Hauoni kwamba kwa Yanga kuruhusu Azam TV waoneshe bure mechi itakuwa ni kuifaidisha Azam TV kutokana na sababu kwamba Azam TV watafaidika na fedha za malipo/gharama za kulipia kuona Azam 1 na 2 pamoja na udhamini wa matangazo hayo ya moja kwa moja(matangazo ya biashara ya bidhaa za SSB)...
 
Hapa ni kuwa challange ili mnunue tickets na mkaangalie
 
Hapa Manji anakuwa janga la mwaka.

Kama issue ni Azam TV watoe haki kwa TBC au Star TV ili mchezo uoneshwe LIVE.
Tatizo sio Azam TV....

Tatizo ni kiasi cha pesa kinachotaka kulipwa...Hauwezi kukubali udhamini wa sh. Milioni 8 au 10 wakati kituo cha Luninga kinapata kiasi kikubwa kutokana na udhamini wa makampuni kwenye hayo matangazo ya moja kwa moja...
 
Tatizo sio Azam TV....

Tatizo ni kiasi cha pesa kinachotaka kulipwa...Hauwezi kukubali udhamini wa sh. Milioni 8 au 10 wakati kituo cha Luninga kinapata kiasi kikubwa kutokana na udhamini wa makampuni kwenye hayo matangazo ya moja kwa moja...

Yaani watoe fedha haitoshi kumsajili hata mchezaji mmoja tu achilia mbali mishahara yake. Timu za waarabu wakiomba kuonyesha kwao live wanalipa zaidi ya pesa hiyo.
 
Mijitu inapenda slope dadaddeki nendeni uwanjani yambafu.
Tv za mikoani wataonesha muende Huko jitu zima unakaa sehemu na maji ya jero ili uangalie game hamna.
Safi sana.
 
Viongozi wengi wa Yanga elimu zao za kuunga unga!

Taja kiongozi mmojawapo wa Yanga mwenye elimu ya kuungaunga kisha unipe kiwango cha elimu cha Geofrey Nyange 'Kaaburu', Evans Aveva, Haji Manara, Zacharia Hans Pope na Said Tully
 
Kama anavyosisitiza Balantanda hapo juu mpira wa sasa ni biashara. Hata ulaya Tv inazilipa timu zinazocheza kiasi cha pesa ili kuonesha mechi. Sasa kama yanga haijalidhika na malipo kuna tatizo gani? Halafu usichukie timi kisa tu mechi haioneshwi, tuweni wazalendo zaidi tukajaze uwanja na kushangilia kwa sana. Yanga Mbele daima..... Nyuma mwiko
 
Back
Top Bottom