Yanga mkitumia hii,kwa Mkapa hatoki mtu mtaenda mbali

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Nyie Yanga ili muweze kusonga mbele CAF tumieni slogan ambayo Simba huwa wanaitumia kwenye mashinda ya CAF

Pia ua galagaza ,iwe mvua au jua ,kwa Mkapa hatoki mtu

Na kama mnaanzia nyumbani lazima mshinde goli zaidi ya 3 ili mkienda away mpambanie droo au mnadundwa tatu moja mnapita kiulaini kwenda hatua inayofuata

Lakini mkileta utopolo mtaishia kucheza Lingala
 
Mpira hauchezwi kwa Slogan, Mpira ni maandalizi mazuri,Mpira unachezwa uwanjani. Yanga wanachotakiwa kujiandaa vizuri, matokeo yatapatikana bila Makelele Wala vitisho. Mpira ni Fair play mpira wa kutishia wapinzani ni mambo ya ujima.
 
Masikini Utopolo na ushamba wa kukwea pipa
Your browser is not able to display this video.
 
Wanaweza wakatangaza Kwa Mkapa hatoki MTU siku mbili kabla wanapeleka mechi CCM Kirumba Mwanza, hapo watajichanganya ndio maana wanaona wapige kimya tu
 
Kwa akili yako unafikiria yao maneno kama war in dar ndio yanayoleta ushindi? Kuna mipango na mikakati mizito sana nyuma yake ili kukamilisha jambo
 
Yanga wakikubali kuvua chupi wakapigwa goli zaidi ya moja kwa Mkapa wamekwisha.
Sijui watalaumu tff au watamlaumu injinia.
 
Yanga wakikubali kuvua chupi wakapigwa goli zaidi ya moja kwa Mkapa wamekwisha.
Sijui watalaumu tff au watamlaumu injinia.
Kuna siku nilikuwa namwambia rafiki yangu mmoja sijui niliwaza nini lakini ghafla tu nikamwambia jamaa kwamba raiti kama timu zetu za Simba na Yanga hazina hali uadui na vinyongo nabwangekuwa timu zenye umoja baina ya wao kwa wao basi huu ndio ulikuwa muda sahihi kwa timu ya Yanga kuifata timu ya Simba na kumuuliza mbinu, mipango na mikakati ambayo mwenzie anafanya mpaka uwanja wa Mkapa umekuwa tishio kwa timu za nje ya nje wanapokuja kucheza na Simba. Lakini kwavile hizi timu zimekuwa na uhahasama kila mmoja anajiona yeye mbabe kwa mwenzio hata kama hana uwezo.
 

Kauli mbiu za nini wakati Mzee Mpili yupo na nazi zimejaa bwetele masokoni..!!
 
Slogan za Manara hizo,Siyo za Simba
 
Kufukuzana kule wakina Manara unafikiri tena Kuna siri hapo.Pakacha limeshavuja hilo.Subiri vipimo hakuna wa kuzuia
 
Kwa akili yako unafikiria yao maneno kama war in dar ndio yanayoleta ushindi? Kuna mipango na mikakati mizito sana nyuma yake ili kukamilisha jambo
Kwa nini wanajeshi wanaimba nyimbo wakijiandaa kwenda vitani?
 
Usidanganywe kuwa simba kiliwapeleka sligans tu,kuna uovu mwingi sana walikuwa wanafanya

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
KWA NN USEMI UKWELI. WAMESHATOLEWA
 
Yanga inashinda kutokana na maandalizi kabambe, na ubora wa kikosi! Sisi siyo watu wa kutegemea slogan, mapaka, au kupulizia dawa za rungu kwenye vumba vya wapinzani wetu kama nyinyi mbumbumbu fc.
 
Yanga inashinda kutokana na maandalizi kabambe, na ubora wa kikosi! Sisi siyo watu wa kutegemea slogan, mapaka, au kupulizia dawa za rungu kwenye vumba vya wapinzani wetu kama nyinyi mbumbumbu fc.

Hakuna kitu kinatia huruma kama Yanga kutolewa hapa hatua ya kindergaten! Matokeo ya mechi ya kwanza tu yatadhihirisha hiki nikisemacho hapa
 
Masikini Utopolo na ushamba wa kukwea pipaView attachment 1893666
Binafsi simshangai sana huyu dogo maana inaweza ikawa si usamba, ila tatizo la kisaikolojia tu. Kuna mchezaji wa Arsenal miaka hiyo alikuwa anaitwa Dennis Bergkamp raia wa Uholanzi, alikuwa yuko radhi atangulie peke yake kwa usafiri mwingine lakini sio ndege
 
Ni kweli Bergkamp alikuwa anakwea treni wanamkuta Munich. Vilevile, ulichosema ni sahihi ndege inaogofya sana wakati wa kupaa hata uwe mzoefu hali hiyo inakutokea. Kwa hiyo, sio sababu ya ushamba wa kutopanda ndege.
 
Wakicheza kwa Mkapa wajue kabisa marefa wanaokuja ni wa kimataifa hivyo ile shaolin wanayocheza ligi kuu halafu marefa wa huku wanajifanya kama hawaioni wakiileta wajiandae kwa kadi nyekundu na penati kwani CAF hakuna kina Bashungwa mfano waliuona cecafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…