Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Mnaiona kama vile Simba haina fowadi wa kueleweka, lakini ndiyo inayoongoza kwa kufunga magoli mengi kwenye Ligi kuu Tanzania. Mnaiona simba kama vile ni timu dhaifu lakini Simba na Yanga zote zilikuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ikashindwa kufuzu hatua ya Makundi, Simba ikafuzu.
Leo Yanga iko kwenye Kombe la Shirikisho wanajisahaulisha kwamba kabla ya kwenda huko na wenyewe pia walikuwa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika wakatolewa. Hivi inakuwaje timu dhaifu ya Simba inaendelea kuwemo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakati timu Imara ya Yanga ilitolewa!!??
Bidii kubwa mliyonayo wanayanga, ombeni pia mjaliwe na nasibu ya kufanikiwa, la sivyo kila siku mtaumwa na mafanikio ya Simba mnaowaona ni timu dhaifu lakini wamejaaliwa sudi njema!!