Yanga msimu ujao club bingwa boresheni point zenu walau zifike 9 sasa tumechoka

Monomer

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2023
Posts
720
Reaction score
1,410
Yanga kwa hii misimu yote iliyocheza club bingwa,Kila msimu kwenye makundi imekua ikimaliza makundi na jumla ya point 8 Kwa match zote 6 inazocheza.Hali hiyo imeifanya yanga kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali mara mbili mtwalia.

Kwa hivyo msimu ujao uongozi wa yanga nafikili Hilo nao pia wameliona kua ni tatizo wanaumiza vichwa kuona namna gani wafanye kuboresha kikosi.Kwa maana hiyo kama bajeti inaruhusu naomba msajili wachezaji wenye maana ili kuondokana na hii aibu ya kila msimu kumaliza na alama 8.

Msimu wa 2023/2024 yanga ilivuna jumla ya alama 8 kwa mchanganuo ufuatao:-
CR belouzedad vs Yanga. 3-0=0
Yanga vs al ahly Cairo 1-1=1
Medeama FC vs Yanga 1-1=1
Yanga vs medeama. 3-0=3
Yanga vs cr Belouzedad. 4-0=3
Al ahly Cairo vs yanga 1-0=0
Jumla 8 hivyo kwakua point zililingana na mpinzani wake belouzedad,head to head ikampeleka yanga robo fainali.

Msimu wa 2024/2025 yanga ilikusanya alama 8 kwa mchanganuo ufuatao:-
Yanga vs al hilal omnduman 0-2=0
Mc Alger vs yanga 2-0=0
Tp mazembe vs yanga 1-1=1
Yanga vs Tp mazembe 3-0=3
Al hilal omnduman vs yanga 0-1=3
Yanga vs mc Alger 0-0=1
Jumla 8 kwakua wengine walikua na zaidi ya alama hizo hivyo yanga ikashindwa kufuzu hatua ya robo fainali.Wakachekwa sana wakaahidi msimu huu kwanza wafuzu hatua ya makundi Kisha hesabu zingine zitapigwa wakishafika makundi.

Msimu wa 2025/2026
Yanga pia imekusanya jumla ya alama 8 kwa mchanganuo ufuatao:-
Yanga vs Far rabat 1-0=3
Js kablye vs yanga 0-0=1
Al ahly Cairo vs yanga 2-0=0
Yanga vs al ahly Cairo 1-1=1
Far Rabat vs yanga 1-0=0
Yanga vs js kablye 3-0=3
Lakini kwakua wengine walikusanya zaidi hivyo yanga kushindwa kufuzu hatua ya robo fainal kwa mara ya pili mfululizo.Mimi kama shabiki wa yanga ambae kila siku nilikua napigizana makelele na watu wa Simba vitendo hivyo vinaniuma sana wakati hapa ndani tumetawala inakuaje nje ligi ya mabingwa tunakua tunasuasua.

Chonde chonde msimu ujao wa 2026/2027 naombeni uongozi japo mkope hela sehemu msajili wachezaji wenye quality ya kuamua match dhidi ya al ahly inakuaje kila msimu nyumbani tunatoa nae draw wakati msimu huu kama tungemfunga basi tungejihakikishia nafasi ya kufuzu kuliko kuanza kuombeana flani afungwe wakati huo anaecheza nae hana cha kupoteza.
 
Hersi alisema lengo la Yanga msimu huu ni kufika makundi wamefikia malengo wewe unaleta mboyoyo
 
Yanga kwa hii misimu yote iliyocheza club bingwa,Kila msimu kwenye makundi imekua ikimaliza makundi na jumla ya point 8 Kwa match zote 6 inazocheza.Hali hiyo imeifanya yanga kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali mara mbili mtwalia.

Kwa hivyo msimu ujao uongozi wa yanga nafikili Hilo nao pia wameliona kua ni tatizo wanaumiza vichwa kuona namna gani wafanye kuboreaha kikosi.Kwa maana hiyo kama bajeti inaruhusu naomba msajili wachezaji wenye maana ili kuondokana na hii aibu ya kila msimu kumaliza na alama 8.

Msimu wa 2023/2024 yanga ilivuna jumla ya alama 8 kwa mchanuo ufuatao:-
CR belouzedad vs Yanga. 3-0=0
Yanga vs al ahly Cairo 1-1=1
Medeama FC vs Yanga 1-1=1
Yanga vs medeama. 3-0=3
Yanga vs cr belouzed. 4-0=3
Al ahly Cairo vs yanga 1-0=0
Jumla 8 hivyo kwakua point zililingana na mpinzani wake belouzedad,head to head ikampeleka yanga robo fainali.

Msimu wa 2024/2025 yanga ilikusanya alama 8 kwa mchanganuo ufuatao:-
Yanga vs al hilal omnduman 0-2=0
Mc Alger vs yanga 2-0=0
Tp mazembe vs yanga 1-1=1
Yanga vs Tp mazembe 3-0=3
Al hilal omnduman vs yanga 0-1=3
Yanga vs mc Alger 0-0=1
Jumla 8 kwakua wengine walikua na zaidi ya alama hizo hivyo yanga ikashindwa kufuzu hatua ya robo fainali.Wakachekwa sana wakaahidi msimu huu kwanza wafuzu hatua ya makundi Kisha hesabu zingine zitapigwa wakishafika makundi.

Msimu wa 2025/2026
Yanga pia imekusanya jumla ya alama 8 kwa mchanganuo ufuatao:-
Yanga vs Far rabat 1-0=3
Js kablye vs yanga 0-0=1
Al ahly Cairo vs yanga 2-0=0
Yanga vs al ahly Cairo 1-1=1
Far Rabat vs yanga 1-0=0
Yanga vs js kablye 3-0=3
Lakini kwakua wengine walikusanya zaidi hivyo yanga kushindwa kufuzu hatua ya robo fainal kwa mara ya pili mfululizo.Mimi kama shabiki wa yanga ambae kila siku nilikua napigizana makelele na watu wa Simba vitendo hivyo vinaniuma sana wakati hapa ndani tumetawala inakuaje nje ligi ya mabingwa tunakua tunasuasua.

Chonde chonde msimu ujao wa 2026/2027 naombeni uongozi japo mkope hela sehemu msajili wachezaji wenye quality ya kuamua match dhidi ya al ahly inakuaje kila msimu nyumbani tunatoa nae draw wakati msimu huu kama tungemfunga basi tungejihakikishia nafasi ya kufuzu kuliko kuanza kuombeana flani afungwe wakati huo anaecheza nae hana cha kupoteza.
Kwa Uchambuzi huu wewe ni Yanga Kufa na Kuzikana. Mwambieni yule Mvulana wenu anayehangaika na Personal Character/Identity atulie na Timu maana kila kitu ni lazima afanye yeye kinachohusu Pesa (10% ale Mwenyewe). Dogo ana Njaa ya Uongozi (Power Monger) since the Precedent of 2025 Election within CCM nilijua huyu is just to "Carp Diem" not otherwise. Anapigwa chini Kigamboni ghafla anaibukia Kongwa what a ***!
Bila Infantinho kumpa kitengo FIFA Tungemsikia anatafuta Ubunge Jimbo la Uvira Uganda.
All in All , Dogo ana leadership skills atulie na moja kama Yanga anaweka PENDING au huko CAF lengo ni concentration & sustainability of an issue.
 
Yanga wanahitaji kujiangalia upya kimataifa, hakuna namna.

Kipindi walipopenya hadi robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na hata kufika fainali ya Kombe la Shirikisho, haikuwa bahati. Ilikuwa ni matokeo ya uwekezaji sahihi, makocha sahihi kama Gamondi na Nabi, pamoja na wachezaji wa kiwango cha juu kama Mayele, Aziz Ki na Fei waliokuwa na uwezo wa kubadilisha mechi.

Lakini Yanga ya sasa imepoteza yale makali, wameridhika na makombe ya ndani. Kocha wa sasa Pedro kaleta mbinu zake za kujilinda kupitiliza “kupaki basi” dhidi anapokutana na upinzani badala ya kwenda kushindana nao kama timu ilivyozoea, Hadi ikafikia hatua viongozi wakaingilia kati wakimshauri abadili mfumo na hata kumletea msaidizi. Hiyo pekee inaonyesha timu ilikurupuka kumleta na ndio chanzo mojawapo cha timu kutofika mbali kimataifa.

Mabadiliko ya makocha kila msimu nayo hayasaidii. Roman Folz aliletwa msimu mpya, wakati tayari kulikuwa na kocha mzuri kama Miloud Hamdi aliyetokea Singida United iliyokuwa moto kuja kubeba mikoba ya Saidi alieimbilia ofa nono ya waarabu, Sead Ramović (Saidi) ukweli ni kwamba Yanga ilimpa jukwaa kubwa zaidi ya timu aliyotokea ya South Africa iliyokuwa mkiani, Lakini inaonekana Yanga aliitumia tu kama ngazi, timu ilipotolewa tu kimataifa, akaomba kuondoka kwenda CR Belouizdad, utadhani alikuwa anaombea timu itolewe aondoke zake haraka kuwahi ofa.

Kwa mwendo huu, Yanga itaendelea kutawala ligi za ndani, Lakini nje ya mipaka hadithi itabaki ile ile: hatua ya makundi, Sasa ni muda wa kufanya maamuzi magumu, kuleta kocha wa muda mrefu mwenye falsafa inayoeleweka, na kusajili wachezaji wa malengo, si wa kubadilishwa kila msimu.

Okello ni mfano mzuri wa hatua za kupata wachezaji wanaoweza kuwa kwenye plan za timu kwa miaka minne, sasa waletwe na wengine hata wawili, Mipango ya kocha mpya ianze sasa, huko alipo awe anajua kuna kazi inamsubiri msimu ujao pamoja na malengo.

Soka la kimataifa halihitaji majaribio, linahitaji mipango, uthabiti na ubora.
 
Mmmh hivi kweli okello ni wakwenda nae akaminyane na al ahly,pyramid,esperanca de tunis,far Rabat,mc Alger,RS berkane mmh mi kwangu Mimi naona hatoshi atasaidia kwa ligi ya ndani lakini sio kuminyana na hao waarabu kidogo depu ndo pakuanzia.
 
Ushauri ni kwa Yanga tu Simba amekatiwa tamaa au yeye katoboa huko kimataifa?
 
Mmmh hivi kweli okello ni wakwenda nae akaminyane na al ahly,pyramid,esperanca de tunis,far Rabat,mc Alger,RS berkane mmh mi kwangu Mimi naona hatoshi atasaidia kwa ligi ya ndani lakini sio kuminyana na hao waarabu kidogo depu ndo pakuanzia.
Okello ana shida gani? niambie weaknesses zake ambazo hizo timu ulizotaja hazina wachezaji wa aina hio
 
Kwanza sio mkabaji pale mnapopoteza mpira basi ujue yeye sio mtu kusuffer kwenda kuuporq mpira kwa adui,nguvu za kuminyana na vijeba hana,kimo pia Cha kuweza kugombania mipira ya juu hakimbebi na Hilo yanga kwa sajiki zijazo wanatakiwa kulifanyia kazi,kwasababu yanga wachezaji wake wengi vimo vyao nivya kati sana.Hivyo kwenye mipira ya Kona tunapata tabu sana kuitumia,kwenye kuzuia,kuzuia mipira ya set pices kwa ujumla.

Kona tunazalisha nyingi sana lakini kuzitumia ni changamoto nyingine sababu kubwa ikiwa ufupi,kuzuia pia ni changamoto rejea afcon juzi tu gamond alilazimika kumuita mwamnyeto kwa kigezo Cha urefu ambae alikua hapati namba yanga.Goli la mtibwa sugar la kuchomoa likitokea kwa Yao kwasi
 
Back
Top Bottom