Yanga na mayele bado ngumu

kipachaibwe

Member
Joined
Dec 11, 2020
Posts
36
Reaction score
71
Kikao kilichofanyika juzi jumapili kati ya uongozi wa Yanga na usimamizi wa Mayele haukufikia muafaka

Yanga wanadai hawataweza kuongeza ofa zaidi kwa Mayele na wamempa machaguo mawili wakala wake

Wametoa siku 5 aidha akubali ofa ya mezani kusaini mkataba mpya

Au auzwe nje ya chi kwa dola laki 9
Sawa na zaidi ya billion 2 kwa pesa ya bongo

Lolote linaweza kutokea
 
nashauri mayele aende tu maana tukimzuia hatacheza kwa furaha

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
Kwani shida iko wapi hasa! Aamue kubaki, au akubali kuuzwa!! Maana Yanga ni zaidi ya Mayele! Ni zaidi ya mtu yeyote yule.Yanga ni wananchi.
 
Wamuuze wakati yupo kwao kwa mkopo 😂😂😂
 
Tatizo ni kwamba wananchi hawawezi kuingia uwanjani kucheza, na hata wakiingia hawawezi kufunga magoli. Hapo ndipo inapoonekana kuwa Mayele ni zaidi ya wananchi
Kwani kabla ya mayele ýanga alikuwa afungi magoli? Wamepita wangapi zaidi ya mayele pale yanga? Akili za kimangungu usiwe unazileta uku!
 
Mayele si bado anamkataba na Yanga wa Mwaka mmoja?
Mbona anashinikizwa kuongeza mkataba wakati mkataba wake haujaisha ?
Nini tatizo hapo Uto?
 
Mayele si bado anamkataba na Yanga wa Mwaka mmoja?
Mbona anashinikizwa kuongeza mkataba wakati mkataba wake haujaisha ?
Nini tatizo hapo Uto?
Kama ni hivyo uto wapo sahihi , Kwa mchezaji muhimu mkataba anaongezewa kabla mkataba mwingine haujaisha la sivyo ataondoka bure.
 
Wachezaji wa Yanga wanaitesa sana yanga.

1)Fei Toto
)Mayele
3)................

Yanga Presha inapanda,
Presha inashuka.
 
Kama ni hivyo uto wapo sahihi , Kwa mchezaji muhimu mkataba anaongezewa kabla mkataba mwingine haujaisha la sivyo ataondoka bure.
Vipi kama anataka kucheza Yanga hadi mkataba wake utakapofikia kikomo?

Mtamlazimisha kumuuza?

Sheria ya mkataba inasemaje hapo?

Nimeajiriwa Yanga kwa miaka miwili, vipi nilazinishwe kusaini mkataba mwingine au kuuzwa kabla ya kutisha mkataba wa awali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…